kwamamaza 7

DR Congo: Wanamgambo wa Jen. Kayumba Nyamwasa watuhumiwa kushiriki katika mauaji ya watu 10

0

Wanamgambo inayotuhumiwa kuwa ni  wa Jen. Kayumba Nyamwasa wanatuhumiwa kushiriki katika mauaji ya watu 10 katika vita vya kikabila kati ya Wanyamulenge na Wafulero, huko Bijombo,eneo la Uvira mkoa wa Kivu Kusini.

Mmoja mwa viongozi wa eneo la Minembwe Gad Mukiza jana amehakikisha hivi vita vimesababisha watu wengi kukimbilia Minembwe.

Taarifa za radiyo Okapi ni kwamba kundi la vijana la Wanyamulenge kwa jina  ‘Twirwaneho’ linapambana na makundi ya makabila mengine yakiwemo Abanyindu, Abafulero na Babembe.

Wakazi wametangazia  radiyo Sauti  ya Marekani kuwa Wanyamulenge wanaungwa mkono na wanamgambo kutoka Rwanda wanaosema kuwa hawa ni Jen. Kayumba Faustin Nyamwasa.

Viongozi wa ngazi za chini wamehakikisha wengi  wameisha kimbia hasa maeneo ya Rubarati, Mbundamo, Masango, Kanogo, Rubibi, Mugogo, Gatoki na Maheta.

Hivi vita vya makabila vinasababishwa na kuwania uongozi na kumiliki mali asili ya hili eneo la Bijombo.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.