kwamamaza 7

Donal Trump amemwambia Theresa kua anakubali kutengana kwa Uwingereza na EU

0

Katika mkutano wake wa kwanza na kiongozi wa kigeni, Rais Donald Trump amesema Marekani na Uingereza “zinauhusiano maalum.”

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekubaliana na hilo, huku akitaja maslahi ya pamoja ya kiuchumi na maadili sawa kuwa ni mfano, lakini pia akasisitiza kuwa rais mpya ameahidi kuisaidia NATO kwa “asilimia 100.”

Trump amesababisha manung’uniko makubwa katika miji ya Ulaya kwa kauli zake kuhusu NATO kuwa imepitwa na wakati na kuwa wanachama wake wanatakiwa kulipa hisa zao kwa ajili ya ulinzi wao wenyewe.

Katika mkutano wa viongozi hao na waandishi wa habari, Trump amesema Uingereza ni nchi iliyoko moyoni wake kwa sababu mama yake anaasili ya Scotland.

“Leo hii Marekani inarejesha upya mafungamano yetu ya dhati na Uingereza- Kijeshi, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Tunauhusiano wa dhati,” amesema rais.

“Tunaahidi kuendeleza mahusiano haya muhimu. Kwa pamoja Marekani na Uingereza ni alama ya mafanikio na utawala wa sheria. Ndio maana Marekani inaheshimu uhuru wa wananchi wa Uingereza na haki yao ya kuamua wanachokitaka. Uingereza iliyo huru na yenye kujitawala ni heri kwa ulimwengu na mahusiano yetu siku zote yamekuwa imara.”

Trump amesema anaiunga mkono Uingereza kwa nguvu zote katika kura ya “Brexit” ilioitoa kutoka Umoja wa Ulaya. “Nafikiri Brexit itakuwa ni kitu kizuri kwa taifa lako,” alisema.

Amesema kuwa Uingereza itaweza kufikia “makubaliano huria ya kibiashara bila ya kusimamiwa na mtu yeyote katika kile mnacho kifanya.”

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.