Home HABARI Dkt. Frank hana uhakika atashiriki mjadala wa wagombea urais kwenye TV
HABARI - SIASA - July 23, 2017

Dkt. Frank hana uhakika atashiriki mjadala wa wagombea urais kwenye TV

Dkt. Frank atangaza kwamba atashiriki mjadala wa wagombea ikiwa tu Rais Kagame Paul naye atakuwepo kwenye mjadala huo unaotarajiwa kupeperushwa kwenye televisheni ya Kituo cha Habari cha Rwanda (RBA).

Kwenye siku za hivi karibuni ndipo Tume ya Uchaguzi ya Rwanda ilipotangaza kwamba kutakuweko mjadala wa wagombea utakaopeperushwa kwenye Radio na TV ya RBA.

Kulingana na habari zinazotangazwa na Moise Bukasa ambaye ni msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Rwanda zinasema kwamba wagombea watapewa nafasi ya kuelezea mipango yao kwa kipindi cha mjadala kitakachokuwa kikipeperushwa moja kwa moja kwenye TV na kukiwa na kiongozi wa mjadala kwenye mjadala huu wananchi watapewa na muda wa kutoa mchango wao kwa kuuliza maswali yao na kutoa maoni kupitia simu zao na hata ujumbe mfupi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Dkt. Frank aliyeitangazia The East African kwamba hajaamua ikiwa atashiriki mjadala ama hatakuweko ila ameongeza kwamba ikiwa Rais Kagame atakuweko naye hatasita kushiriki mjadala huo.

Inasemekana kuwa Rais Kagame naye atakuwepo pekee yake kama msimamizi wa chama cha RPF kilichomteua kuwa mgombea kwa tiketi yake, kwenye mjadala huo utakaokuwa ukifanyika kwa mara ya kwanza ya historia ya uchaguzi ya Rwanda.

Wagombea watatu ndio wanaowania kiti cha urais wa Rwanda katika uchaguzi mkuu unaofanyika mwezi ujao tarehe 4. Wagombea hao ni Paul Kagame anayewania urais kwa muhula wa tatu, Dkt. Frank Habineza wa chama cha Green halafu Mpayimana Phillipe ambaye ni mgombea huru pekee wa uchaguzi huu.

Shughuli za kampeni zilizoanza tarehe 14 Julai zinaendelea ikiwa zinatarajiwa kumalizika tarehe 3 na uchaguzi siku moja baadaye tu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.