Home HABARI MPYA Dkt. Frank Habineza na imani kubwa ya kushinda uchaguzi kwa asilimia 51%
HABARI MPYA - SIASA - June 28, 2017

Dkt. Frank Habineza na imani kubwa ya kushinda uchaguzi kwa asilimia 51%

Baada ya Tume ya Uchaguzi kuwatangaza wagombea halali wa muda, Dkt. Frank Habineza ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya chama chake cha Green ametangaza kwamba watashinda uchaguzi kwa asilimia 51% kama vile alivyotangaza awali.

Dkt. Frank Ametangaza hivi baada ya kutangwaza na Tume ya Uchaguzi kama mgombea rasmi wa muda pamoja na Paul Kagame wa RPF wakati kukitarajiwa wagombea rasmi kutangazwa hapo tarehe 7 Julai.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Prof Kalisa Mbanda ametangaza jana tarehe 28 Juni 2017, kwamba wagombea hao wawili ndio hadi sasa wamekubaliwa kwa muda wakati ambapo wagombea wengine binafsi wamekataliwa.

Hata hivyo, Prof Mbanda ametangaza kwamba kilichowafanya kutokubaliwa ni upungufu wa idadi ya wafuasi ambao hakuna yeyote anayezaja idadi kamili ya wafuasi 600 kutoka nchini kote.

Wagombea hao ni Mpayimana Philippe, Mwenedata Gilbert, Barafinda Sekikubo Fred na Rwigara Diane ambao ugombea wao hauko halali.

Aidha Prof Kalisa Mbanda amesema kwamba wagombea hao wana muda hadi tarehe 6 Julai kujaza yangali yanakosekana kwenye nyaraka zao wakisubiri tarehe 7 Julai kutangazwa kwa wagombea rasmi watakaowania kiti cha urais katika uchaguzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Akihojiwa na Bwiza.com Dr. Frank Habineza, ametangaza kufurahia kauli ya NEC yeye kama Mwenyekiti na wafuasi wengine wa chama chake. Kusalia kwa wagombea wawili kwa muda siwezi kusema ndio inayotupa uwezekano wa kushinda uchaguzi, tulikuwa bado na bahati ya kushinda uchaguzi kwa aslimia 5.

“tulikuwa na uwezekano wa kushinda uchaguzi kwa asilimia 51 hata awali” asema

Wakati alipoongea katika kipindi cha redio moja ya hapa nchini, walimwuliza Dkt. Frank ikiwa haoni uwezekano wowote wa kushindwa uchaguzi na alikiri kwamba yote yanawezekana na watakubali matokeo ikiwa hakuna mfuasi wa chama cha Green atakayekuwa ameonewa.

“yote yanawezekana, katika siasa ya Kidemokrasia kuna kushinda na kushindwa na tutakubali matokeo wakati wowote ambapo hakutakuwa na mfuasi wetu ambaye amepigwa, ameteswa, amezuiwa, ama kuuliwa ama kuihama nchi kwa sababu ya mawazo yao, lakini wakati kutakuwa na mtu yeyote awe kutoka chama kingine ambaye atakabili hali hii uchaguzi hautakuwa wa huru na haki”

Aliendelea kusema kwamba wanataka uchaguzi kufanyika kwa huru na haki, bila kuwepo kwa mfuasi ambaye ataonewa na kusema zaidi kuwa kuna wafuasi wa chama chake wanaoteswa kutoka vijijini kadhaa vya nchi.

Uchaguzi utafanyika tarehe 3 na 4 mwezi Agosti 2017.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.