kwamamaza 7

Dkt.Frank Habineza: Malipo ya juu ya kodi pingamizi kwa biashara ya Rwanda

0

Katika mahojiano na Bwiza.com, mwanasiasa huyu, mwenyekiti wa chama cha Green, DPGR amesema kwamba gharama ya kodi ni kali kwa kiasi cha kutorahisisha uendeshaji biashara mzuri.

Alipoulizwa msimamo wa uchumi wa Rwanda kulingana na nchi za Kimataifa, amejibu kwa mara kwamba wafanyabiashara wadogo wa Rwanda hawako katika hali nzuri kwa sababu ya gharama ya kodi iliyo juu na hata bei ya kupanga nyumba isiyo rahisi.

Akihojiwa kuhusu msimamo wake kuhusu kodi amesema kwamba kodi ni lazima ilipwe lakini inapaswa kulipwa kulingana na kiwango cha biashara na mapato yake lasivyo biashara nyingi huanguka au wamiliki wake huhamisha biashara zao katika nchi za ng’ambo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hapa ametoa mfano wa nyumba nyingi zilizoko mjini Kigali akisisitiza kwamba zimekosa wapangaji kwa hofu ya malipo ya kodi na hata bei ya kupanga iliyoko juu.

Amependekeza ulipaji kodi unaozingatia ukuaji wa biashara ama progressive taxation kama suluhu la suala hili.

Amegusia hapa upiganiaji masoko, na akasema kwamba huwa anapewa watu maalum na kwa hili amewashtumu chama cha RPF ambacho kinatawala na kuongeza kwamba huwa vigumu kikitofautisha na serikali. Kwa mjibu wake haifai kwa vyama vya siasa au serikali kushiriki katika shughuli za biashara.

Akihojiwa ikiwa kupunguza kodi hakungeathiri maendeleo ya nchi ambayo inategemea sana mapato ya kodi, amesema kwamba kodi ingepunguzwa na kwa hiyo wafanyabiashara walipaji wa kodi wangeongezeka kwa wingi na hivyo mapato ya kodi akaendelea kuwa yale yale.

Dkt. Frank Habineza, ni mojawapo wa wagombea waliokwisha asilisha nyaraka zao kwa ajili kushindana katika uchaguzi wa rais wa hapo Agosti mwaka 2017. Atakuwa akigombea kwa tiketi ya chama chake Green (DPGR).

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.