kwamamaza 7

Dkt. Frank Habineza ana imani kwamba waliochagua katika referendum watamchagua

0

Mwenyekiti wa chama cha upinzani wa serilikali ya Rwanda Dkt. Frank Habineza amewasilisha nyaraka zake kwa tume ya Uchaguzi ili aweze kupata ruhusa ya kuwania kiti cha urais wa kuitawala Rwanda na ana imani atapata waungamkono wengi.

Mnamo saa nne za siku ya jana ndipo Habineza alipowasilisha nyaraka zake kwa tume ya uchaguzi huku akisindikizwa na viongozi wenzake wa chama hicho. Miongoni mwa nyaraka alizompa Kiongozi wa tume hii, Prof. Kalisa Mbanda amekuwa akikosa kadi ya uchaguzi ambayo amehimizwa kuitafuta.

Akijibu hoja za waandishi wa habari amesema kwamba ugombea wake ukikubaliwa atapata waungamkono wengi.“ Chama chetu kinanataka mabadiliko, ni chama cha upinzani ambacho tuliunda mwaka wa 2009, kwa sasa tuna uezekano wa kushinda zaidi ya 51%” amesema .

Ameendelea kusema kwamba Green Party haikuunga mkono marekebisho ya katiba na walipiga marufuku watu kuchagua ndio katika referandamu.

Green Party wanatarajia kupata kura za waliochagua katika referendamu

“ Tuna imani tutashinda uchaguzi, Tume ya uchaguzi ilituarifu kwamba kuna zaidi ya wapiga kura zaidi ya milioni wapya waliojiandikisha na ambao hawakupiga kura katika referandamu hao wote watatuchagua.” Dkt. Habineza asema.

Wengine ambao amesema watamuunga mkono ni wanachama wa vyama ambavyo vilitangangaza hivi karibuni kuwa vitamuunga mkono rais Kagame.

Amesema pia kuwa wao waliona kwamba si tabia nzuri ya kidemokrasi ambako Rwanda ni serikali yenye mfumo wa vyama vingi. Tunajua baadhi yao hawakuunga mkono kurekebishwa kwa katiba, kwa hivyo tutawashawishi kutuunga mkono.

Green Party yaahidi mabadiliko.

Green Party inapanga kuleta mabadiliko mengi ikiwemo katika jinsi ya utawala wa Rwanda, elimu, afya, usalama nakhadhalika.

“ Kwa kweli tunawaahidi kuanzisha mifumo ambayo itawezesha upatikanaji wa chakula cha kuridhisha. Tutatilia maanani hata elimu bora kwa sasa serikali haikujenga misingi yake na elimu bora inaonekana kuwa na matatizo” .asema.

Wanyarwanda watasaidiwa kupata ada na msaada wa kufuata elmu ya vyuo vikuu.

Green party kuanzisha mahakama mpia

Kuna matatizo mengi katika sekta ya kilimo, ya elmu , ya sheria na usalama. Katika sheria kuna tatizo kubwa sana kwa kuwa hatuna mahakama ya kutunza katiba, hiyo tutaianzisha na tutaondoa magereza ambayo anawafunga watu kinyume na sheria.Walinda magereza watapewa mafunzo maalum ili kuepukana na tabia ya kuwafyatua watu kiholela.

Katika usalama kutaanzishwa idara ya usalama na majeshi kujengewa malazi kwa kuwa kwa hivi wanalala tu kwenye hema.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kuna wakati wasingekubali matokeo ya kura

Dkt. Habineza amesema kuwa wana imani uchaguzi utaenda vizuri lakini pia akasema kwamba ungalikuwa mbaya hawangekubali matokeo.

“Tunadhani Tume itaendesha shughuli za uchaguzi ipasavyo, na wangefanya kinyume na hivyo, wakatutesa, wafuasi wetu wakapigwa, wakafungwa wakati huo hatutakubali matokeo na tutafuata njia ya mahakama” asema.

Lakini iwapo uchaguzi utaendeshwa kwa haki na wagombea wakapewa nafasi sawa za kujieleza katika vyombo vya habari wakati wa kampeni, ‘tutakubali matokeo’ la hasha tuna imani ya tutashinda uchaguzi.Isipokuwa Green Party na RPF hakuna Chama kingine kinachotarajiwa kumtoa mgombea.

Na upande wa wagombea binafsi Mwenedata na Barafinda Sekikubo Fred wamekwisha asilisha nyaraka zao kwa Tume ya Uchaguzi. Kunasubiriwa Shimwa Rwigara Diane na Mpayimana Philippe kuasilisha nyaraka zao.

Orodha ya wagombea rasmi itatangazwa tarehe 7 mwezi wa Saba 2017 kukikosa mwezi mmoja hadi uchaguzi kufanyika hapo tarehe 3 na 4 mwezi wa nane.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.