kwamamaza 7

Dkt. Frank ashindwa kuendesha kampeni zake za uchaguzi Nyagatare

0

Ikiwa imekuwa ikitarajiwa kwamba shughuli za kampeni za mgombea wa chama cha Green, Dkt. Frank Habineza, kuendeshwa kwenye wilaya ya Nyagatare na baadaye Gatsibo na mwishowe shughuli zake wilaya ya Nyagatare zikafeli kufuatia kubadilishwa kwa mahali palipokuwa pakitarajiwa kuendeshwa kampeni na hata vurugu za waendesha pikipiki.

Wafuasi wa chama cha Green wamedai kwamba wametatizwa na viongozi wa tarafa ya Rwimiyaga kwa sababu waliomba mahali pa kuendesha kampeni na wakakataliwa kwa madai ya kwamba ni karibu na soko. Baada ya hayo wakaaumua kahamisha kampeni zao kwenye kijiji cha Rwimiyaga na wakajikuta wameagizwa kwenda Bugaragara ambapo wanachama wanasema wameona kwamba ni karibu na makaburi na wakakataa kuendesha kampeni hapo.

Hata hivyo Sylver Ruboneka, Katibu Mtendaji wa tarafa ya Rwimiyaga amekana kumtatiza  mgombea Frank na kusema kwamba mahali walipoagizwa kuendesha kampeni ni mahali penye kiwanja panapofanyiwa kwa kawaida mikutano ya jamii.

Alipoongea na vyombo vya habari mgombea Frank alipendekeza serikali ya Rwanda kuwachukulia hatua viongozi hawa ikiwemo kuwaondosha uadhifani.

“Jambo la kusitikisha ni kwamba walitupeleka mahali penye makaburi na tukaona hatuna sababu ya kugombana, hatukimbii matatizo, tunapambana nayo lakini tungetaka serikali MINALOC kulaani yaliyofanywa na viongozi hawa kwani kitendo hiki ni kinyume na kanuni za kura na demokrasia iwapo sisi wote tuko wagombea halali na kwa hivyo tunaomba viongozi hawa kuondolewa uadhifani”

Kuhusu mzozo wa waendesha pikipiki, mgombea huu alisema, “Tulipoamua kuzunguuka barabara tukiwapepea wananchi tulipoona waendesha pikipiki wakisambaa barabara tulidhani kuwa wamekuwa wakija kutushangilia kumbe wamekuwa wakikusudia kuzua mzozo na tukaamua kuwa tulivu na polisi ikajitokeza kusaidia”

Baada ya shughuli zake kutofanyika kama ilivyokuwa ikitarajiwa Mgombea huu aliendelea na shughuli zake kwenye wilaya ya Gatsibo eneo la Kabarore.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.