kwamamaza 7

Dkt. Frank aahidi kumaliza tatitizo la njaa eneo la Bugesera

0

Huu ni mojawapo ya mipango aliyoasilisha kwa raia wa Bugesera wakati alipokuwa akiendesha kampeni za kusaka kura katika uchaguzi utakaofanyika hapo tarehe 4 mwezi Agosti.

Dkt. Frank ameahidi kutolea suluhu la kudumu matatizo yaliyowakumba raia wa Bugesera. atangaza haya siku ya jana tarehe 4 Agosti , alipokuwa mbele ya raia wa Bugesera kwenye tarafa ya Juru.

Miongoni mwa mengine aliyoahaidi ni pamoja na kupambana na tatizo la ukame lililokumba eneo hili kwa kutumia maji ya mto Akagera kwa kumwagia mimea kusiko kuyaacha yakaenda kuwanufaisha wamisri tu ambako amesema ni tegemeo la maisha ya wamisri wapatao milioni 80.

Amesema pia kwamba atawarudishia raia wa eneo hilo ardhi ya mashamba oevu yaliyopewa raia wa nchi za kigeni ili waweze kuyazalisha mali na kuyalima wakati wa kiangazi.

Amedokeza kuhusu fidia waliopewa wamilki wa mali iliyokuwa kwenye mahali palipotengwa kwa ajili ya kujenga kiwanja cha ndege na kuwaahidi kwamba iwapo atachaguliwa atawafidia kulingana na thamani ya mali yao.

Jambo jingine alilosema akiwa anaeleza mipango yake ni kuhusu kodi ya mashamba wanaolipa wananchi licha ya kuwa mali yao ni ya kiasili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Frank amewajibu wanao mashaka ya kuwa yatakuweko na uwezo wa kutekeleza ahadi zake iwapo atachaguliwa kuwa rais. Hapa amesema kuwa Rwanda haijakosa fedha za kuwekeza kwenye mipango ya kuendeleza nchi na raia wake kwa kuwa na mkaguzi wa mali alitangaza kwamba asilimia 40 ya bajeti imeporwa na Mkaguzi mkuu wa mali aliwatangaza wahusika hawakufuatiliwa kisheria ila tu “samaki wadogo”.

Kupambana na hili Dkt. Frank amesema ataondoa njia zote za rushwa na kuacha fedha hizo kutumiwa kwa shuguli muhimu za nchi.

Alisema pia kuwa Rwanda ina maliasili nyingi ambazo hazijatumiwa bado ikiwemo mafuta na amesema kuwa iwapo zitaanza kutumiwa fedha zitaongezeka ila na zile zinazopatikana zingali zinafaa kwa kukidhi shughuli za maendeleo za nchi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.