kwamamaza 7

Diane Rwigara amewasilisha nyaraka zake kwa tume ya Uchaguzi

0

Mwanadada, Shimwa Rwigara Diane amewasilisha nyaraka zake kwa Tume ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC).

Nyaraka alizowakilisha kwa tume ya Uchaguzi ni pamoja na hati ya kuzaliwa,ya uraia,kadi ya uchaguzi, na hati ya kuthibitisha kwamba hajahukumiwa na mahakama kifungo zaidi ya miezi 6 na saini mia sita za wafuasi wake 600 ambazo kila mgombea anahitajika kupata na nyaraka nyinginezo

Katika mahojiano na wanahabari, mwanadada huyu alisema kwamba wafuasi wake waliomsadia kupata saini wamo hadi sasa katika hatari ya usalama. Amesema zaidi kwamba moja wao hawalali makwao na kwamba alikwisha ripoti kesi hii kwa Polisi na Kamati ya Uchaguzi ila mpaka sasa hajapata jibu lolote.

Alisema kwamba imani yake ya kushinda uchaguzi inalingana na sababu kwamba kunatakiwa mabadiliko nchini Rwanda.

“ nina imani kwamba nitashinda uchaguzi kwa sababu tunataka mabadiliko kila mnyarwanda anuunga mkono mabadiliko” Asema Rwigara Diane

[xyz-ihs snippet=”google”]

Shimwa Rwigara Diane mwanadada binti yake marehemu mwenyemali Rwigara Assinapol ni mgombea kike pekee aliyetangaza nia yake ya Kugombea urais katika uchaguzi mwa hapo Agosti 2017.

Ugombea wake unafuatia ule wa wagombea wengine wakiwemo Dkt. Frank Habineza wa Chama cha Green, na Mwenedata Gilbert ambaye ni mgombea binafsi.

Tarehe ya mwisho ya wagombea kufikisha nyaraka zao kwa Tume ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC) ni 27 Juni na watasubiri hadi tarehe 07 Julai, ambapo wagombea rasmi watatangazwa na tume ya Uchaguzi na Shhughuli za kuendesha kampeni zikaanza tarehe 14 Julai.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.