Dhambi ikishakukolea, na rafiki yako shetani alishajua hapa hatoki mtu. Atakachokifanya ni kukupandikiza chuki ndani yako.

Hii chuki sio ya kuichukia hiyo hali uliyonayo, bali ni kuwachukia watumishi au wachungaji wa Mungu.

Mchungaji ao mtumishi wa Mungu akihubiri ujumbe ambao unagusa maeneo yako machafu, cha kwanza kitakachokujia kichwani… ni huyu mtumishi atakuwa ameambiwa habari zangu au ni kama mchungaji wako wa kila siku utaona anakusema wewe.

Hii roho ya chuki inajenga mizizi zaidi, ukiona huyo mtumishi amesimama au ukauona ujumbe wake. Kuna kasauti katakunong’oneza amekuja na yale yale tena.

Nia haswa ya kupandikizwa hii roho ya chuki sio kana kwamba ni hali ya kawaida, bali ni hali ya kuendelea kukumiliki uendelee kuwa mwanafunzi wa Shetani.

Ambapo ni tofauti kabisa na mwanafunzi wa Yesu asikiapo neno la Mungu lenye kugusa maeneo yake ambayo aliona yupo sawa kumbe hakuwa sawa, hujirudi na kurekebisha haraka na kutubu mbele Mungu.

Ukijiona una katabia cha kupenda sana mahubiri ya mapesa, majumba, maghorofa na cheo… alafu yakifika yale mafundisho yenye kukuonya uache dhambi, badaya yake wewe unachukia na kuona huyu mtumishi amekosa ujumbe kabisa mzuri… Ujue una ufa sehemu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Chuki ya kuhisi neno la Mungu ni kama kukupotezea muda, ni mbaya sana ya kukufanya uendelee kuwa na giza la kutojua kweli. Unayo nafasi ya kujitathimini upo kundi la mwanafunzi wa nani, kati ya mwanafunzi wa Yesu au mfuasi wa Ibilisi.

Wanaopendelea bwiza.com iwatembelee na kuwatangazia habari kwenye bidhaa vyao wanaweza kutumia ujumbe kwenye barua pepe ya meckypro@gmail.com, ama wapigie simu kwenye nambari ifuatayo: 0784685981.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.