kwamamaza 7

Dalili 7 za kuonyesha ama mwanamke mwenye aibu anakupenda

0

Wanaume wengi mara nyingi kama wanatongoza wanawake wanashughulika sana na wale ambao wanajiamini zaidi na kusahau kwamba kuna wale ambao kawaida wana tabia za kuwa na aibu. Tabia za mwanamke mwenye aibu ni yule ambaye mara nyingi anaogopa kujionyesha kwa umma, ni yule ambaye hapendi kujihushisha na maswala ya wengine na hupenda kufanya mambo kivyake vyake. Mara nyingi aina hii ya mwanamke husahaulika au kutoshughulikiwa na wengi.
Ukweli ni kwamba wanaume wengine huona ya kwamba mwanamke ambaye anajiamini mara nyingi huvutia zaidi wakisau ya kuwa kama mwanamke yeyote, wanawake wenye aibu pia wanapendeza. Mwanzo wanaweza kupendeza zaidi kushinda hata wanawake wengine ni vile tu hawapendi kujionyesha.
Mimi ningetoa ushauri kwa mwanamume yeyote ambaye hanaconfidence ya kumtongoza ama kuapproach demu ambaye si ligi moja naye, ingekuwa vyema kujaribu kwa mwanamke ambaye ana haya. Hii inasaidia mwanamume yeyote kujiamini zaidi kuliko wakati wowote ule anapotongoza mwanamke aina nyingine.
Tukirudi kwa mada yenyewe ni kuwa utajuaje kama mwanamke mwenye haya amekuzimia ama anakupenda? Kwa kawaida inakuwa vigumu kwa mwanamke aina hii kukuambia kwa mdomo kuwa anakupenda lakini kuna dalili huwa anakuashiria kuwa anakupenda. Dalili zenyewe ni kama zifuatazo:

1. Kukuangalia
Mwanamke kukuangalia kwa muda mrefu bila kuangalia kando ni dalili moja kuonyesha kuwa anakupenda. Hii pia hufanyika kwa mwanamke ambaye ana aibu. Ukihakikisha kuwa mwanamke aina kama hii anakuangalia wewe na wala si mwingine kwa muda ujue hio ni moja wapo ya dalili ya kukupenda. Ukimwangalia halafu kwa ghafla aangalie kando itakuwa ni ishara ya zaidi kuwa anakupenda. Hakikisha kuwa akikuangalia wewe mrudishie kwa kumwonyesha tabasamu. Hakikisha kuwa kama unamwangalia, usiangalie kando mpaka yeye aanze kuangalia kando. Ukiangalia kando wa kwanza utadhihrisha kwake kuwa hujapendezwa naye hivyo kumfanya yeye kuingiwa na aibu zaidi ya kujaribu kueleza hisia zake kwako.

 1. Anapenda kukuonyesha tabasamu/smile zaidi kwako kuliko kwa wengine
  Kuelewa hisia za tabasamu kwa mtu ni jambo gumu sana katika binadamu. Kutabasamu kunaweza kumaanisha kitu na pia kunaweza kusimaanishe chochote. Kama mimi ni wewe nikiona mwanamke akinipa tabasamu sitarukia kuanza kuingiwa na mawazo ya kuwa ananipenda. Kile ambacho nitafanya ni kumakinika na vile ambavyo anatabasamu. Je tabasamu hilo analipeana kwa kila mtu ana ni specially kwangu. Na je aina ya tabasamu hilo likoje.
  Kwa mwanamke ambaye ana aibu, kutabasamu kunaweza kuwa ni tabia yake ya kila siku lakini kile ambacho utamakinika nacho nikuangalia tabasamu hilo analiweka vipi. Wakati akikupa tabasamu, hakikisha kuangalia miondogo yake ya midomo na pia yaangalie macho yake kwa undani. bila shaka kama anakupenda utangundua mara moja.

  3. Anapenda kucheka wakati unapofanya ama kutoa mizaha/jokes zako
  Ok labda wewe ni mtu mcheshi ambaye hakupiti neno moja bila kuchekesha watu. Kila mtu anakujua wewe ni mcheshi lakini kuna huyu mwanamke mwenye aibu ambaye kila neno utakalotoa lazima yeye acheke. Hata kama umetumia maneno ambayo hayachekeshi kabisa bado utamwona akicheka. Hapa kuna vitu viwili ambavyo vinaweza kuashiriwa. Anaweza kuwa ni naturally kuwa yeye anapenda kucheka ama amekuzimia na amependezwa nawe.

 2. Anapenda kukugusa ama kukushika kwa bahati mbaya mara kwa mara
  Kama anapenda kukugusagusa mara kwa mara wakati anapoongea itakuwa ni habari njema kwako. Wanawake kwa kawaida wanajitambua kwa miili yao na kawaida wanapenda kuwagusa wale ambao wanawapenda. Kama anapenda kukugusa kwa mabega kwa bahati mbaya hii ichukulie kama ishara ya kuwa mwanamke kama huyu anakupenda kwa kiasi fulani.
  Onyo: Kuwa makini, hata kama mwanamke kama huyu ni mwenye aibu na mara kwa mara anapenda kukukumbatia, inaweza labda kumaanisha tofauti kabisa. Labda mwanamke kama huyu amejenga ukuta wa kukufanya wewe rafiki yake pekee. Yaani kwa kimombo tunaita ‘friend zone’. Anaweza kukueleza mambo yake yote huku akilini mwake akijua kuwa wewe ni rafiki yake thabiti na hauwezi kuwa mpenzi wake
 3. Anapenda kuongea na kila mtu isipokuwa wewe
  Hii ni tabia halisi ya mwanamke mwenye kuona aibu. Wakati mwingine mwanamke aina hii huona aibu kwa mtu mmoja tu na kwa wengine anakuwa mtu wa kawaida. Ushawahi kumgundua kuwa kwa watu wengine anakuwa huru kuongea nao lakini akifika kwako anaingiwa na aibu nzito.
  Hili ni jambo la kawaida ambalo hutokea kwa wanawake, labda hataki kuongea na wewe kwa kuwa na uoga wa kuongea kitu ambacho kitamuaibisha ama kuongea mambo ambayo utayaona hayafai. Pia labda atakataa kuongea na wewe ili kukuona una wivu kiasi gani akiwa anaongea na wanaume wengine.

  6. Anakuwa na tabia isioeleweka
  Ushawahi kumwona akiangusha vitu vyake kwa sakafu kwa bahati mbaya ama kuonyesha tabia nyingine za kutatanisha? Ashawahi kukuuliza maswali ya kijumla huku akijua wazi huwezi kuyajibu? Wakati anapoongea na wewe wakati mwingine ushawahi kuongea mambo kumhusu ambayo anayafanya kama ni lazima kwa maisha yake? Ama kwa kawaida anapenda kuongea na sauti kubwa lakini pindi unapotokezea anabadilisha sauti nk?
  Dalili hizi zote zinamwonyesha kuwa ameingiwa na wasiwasi akiwa karibu yako.

  7. Anapenda kujichunguzachunguza
  hivi anajaribu kujipendekeza kwako kuonekana kama hana tatizo lolote vile alivyovyaa. Utamwona mara kwa mara akijishika nywele zake ama kuivuta nguo yake ili ionekane imekaa vizuri ama kushika miwani yake mara kwa mara. Kila kitu ambacho anafanya ni kuhakikisha kuwa kinaoneka vizuri machoni mwako.
  Kama wataka kujua mwanamke amekuzimia haswa mkiwa date pamoja atakuwa kila ya madakika akienda msalani kujiangalia kwa kioo kuhakikisha ya kuwa anaoneka mrembo akiwa mbele yako

 

 1. Kila mahali uendapo atakuwa hapo
  Anakula hoteli unayoenda, anapenda kuwa karibu na marafiki zako, na parties zote utakazoenda atakuwa hapo. Tabia ambazo uzianza mpya kwa ghafla utamwona mwanamke kama huyu amekuwa nazo. Wakati ambapo kila mtu atakuwa ameenda, yeye atakuwa wa mwisho ili mradi awe karibu yako.
  Dalili hizi zote zinaweza kutokea kwa nyote wawili kwa bahati mbaya lakini kama zitatokezea na baadhi ya dalili nyingine za kushuku, basi itakuwa mwanamke huyu anafanya hivyo ili kukuona umeridhika na amekupendeza.

  Kumalizia ni kuwa mwanamke kama huyu inaweza kuwa vigumu kumwelewa sababu mara leo atakuwa hivi ama kesho ageuke hivyo ukipata nafasi kama hii ukiona anakuzimia ama kuonyesha dalili zozote, hakikisha ya kwamba haupotezi nafasi yoyote ile kwani hatabiriki kwa urahisi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.