Swahili
MICHEZO

Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya nne ya Ballon d’Or

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or 2016 hii ikiwa ni kwa mara ya nne.

Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.

”sikuwahi kuwaza kama ningeshinda Ballon d’Or mara nne” nina furaha kubwa sana, najisikia fahari. Natumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji wenzangu, timu yangu ya taifa, makocha na watru wote walionisaidia kupata tuzo hii.” Alisema Ronaldo.

[ad id=”72″]

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.

Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.

Kwa sasa ameshinda Ballon d’Or 2008, 2013, 2014 na 2016 na tokea mwaka 2009 amekuwa akipokezana na Messi.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amefunga magoli 19 katika michezo 20 kwa klabu na timu ya taifa msimu huu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com