kwamamaza 7

Cristiano Ronaldo ajibu madai ya udanganyifu wa kodi

0

Kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter “ kuna wakati inakuwa bora kukaa kimya” Ronaldo amejibu madai ya kudanganya kodi baada ya muda kutokuwa na neno.

Jumatanu hii ya tarehe 13 ndipo mwendesha mashtaka wa Uhispania alipowasilisha madai ya kumushtumu mshindi wa mipira mine ya dhahabu(ballon d’or) kwa mahakama ya Pozuelo kwa kuvunja kwa hiari na kwa kufahamu masharti ya kodi.

Madai hayo yanamshtumu “kujenga mfumo wa kibiashara” mwakani 2010 kwa ajili ya kuficha mapato yanayotokana na hakimilki ya sura yake kutoka 2011 hadi 2014.

Hata hivyo, Gestufe- kampuni ya wakala wake, George Mendes imeweka wazi nyaraka zote za kueleza jinsi malipo ya kodi ya hakimilki ya sura yalilipwa na kusema hakuwa na kitu chochote kilicho fichwa na hakuwa na makusudi yoyote ya kuficha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Real Madrid imemuunga mkuno na kusema kuwa hatapatikana na hatia. Kiungo huu wa Real Madrid, mwenye umri wa mika 32 anamiliki ballon d’or nne na kuna uezekano mkubwa kwamba atashinda ballon d’or ya tano baada ya kusaidia timu yake ya Real Madrid kuibuka mabingwa wa Champions League na La Liga. Kiungo huyu aliweza pia kushinda magoli jumla ya 12 kwa mashindano ya Champions League.

Ronaldo anafuatiliwa mahakamani baada ya Messi kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 mwaka jana kwa mashta kama haya.

 

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.