kwamamaza 7

Conte afanya kosa la kuiafiri Chelsea kwa kumtumia ujumbe Costa

0

Antonio Conte alifanya kosa ambalo huweza likaafiri Chelsea na hata wachezaji baada ya mshambuliaji wake Diego Costa kuweka wazi kwamba amefahamishwa na meneja kuwa hayuko tena katika mipango yake.

Kwa mjibu wa habari hii kutoka bbc.com,Costa, 28, mshambuliaji ambae alifunga mabao 20 katika emchi 35 alizocheza Ligi ya Premia na kusaidia Blues kushinda taji la ligi hiyo lakini sasa anaonekana kukaribia kuondoka Stamford Bridge baada ya kufunguka kuhusu ujumbe aliomtumia meneja, inaonekana huweza ikaafiri hata timu.

Costa alisema kwamba ni mchezaji wa Chelsea lakini meneja hamtaki.

Mengi kuhusu ujumbe huu ni kwamba meneja amewatumia ujumbe wachezaji wote akiwatakia likizo njema na kuwatakia wabaki imara.

Costa alimjibu kwa utani na baadaye Conte kumwandikia

“Hujambo Diego ahsante kwa msimu tulioshinda pamoja. Nakutakia heri katika msimu ujao lakini hauko kwenye mipango yangu”

Diego Costa aliupeleka ujumbe huu kwenye bodi la Chelsea ili waamue na akatumia hata wachezaji wenzake.

Akiongea na vyombo vya habari Costa alisema kwamba Uhusiano wake na meneja haukuwa mzuri na kuongeza kwamba ikiwa meneja hamtaki ni lazima atafute timu ya kuichezea

Costa anasema angependa kurudia Atletico Madrid ambako alitoka baada ya kunuliwa na Chelsea fedha zinazokadiriwa kuwa karibu ya millioni 32 £ mwaka wa 2013. Lakini pingamizi ni kwamba Atletico Madrid imewekewa vikwazo vya kusajili wachezaji na angepaswa kusubiri hadi miezi mitano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Je ujumbe wa Conte utaifiri Chelsea vipi?

Ujumbe huu wa Conte ni kosa ambalo bila shaka litaifiri Chelsea wala si katika soko la usajili si hata katika uhusiano wa wachezaji na meneja.

Wachmbuzi wa Soka wansema kwamba meneja kuonyesha kwamba hamtaki Costa, ni kuonyesha hali ya kumdhunisha kithamani ni hivyo itamfanya kununuliwa kwa pesa ndogo.

La pili itakuwa vigumu kwa Chelsea kumpata mshambuliaji wa kujaza pengo litakalokuwa limeachwa.

Mshambuliaji huu alikorofishana na meneja wa mazoezi mwezi Januari na akaachwa nje ya kikosi kilichosafiri kucheza na Leicester City.

Baadaye kulifuata tetesi kuwa huenda Costa akeenda kucheza China ambako kulikuwa na timu iliyompa ofa yenye mshara wa 30£.

Mpaka sasa hatima ya Diego Costa yaijafahamika kwa kuwa uwezekano wa kuchezea China umepata pingamizi baada ya hatua za kuwapunguza idadi wachezaji kutoka nje ya China. Na klabu ya Tianjin Quanjian ilisema kwamba imebadili nia yao ya kumsakaka Diego Costa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.