Swahili
Home » COMESA Kupeleka waangalizi wa kura Rwanda na Kenya
SIASA

COMESA Kupeleka waangalizi wa kura Rwanda na Kenya

Kulingana na Tangazo la Shirika la Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki na Kusini ni kwamba waangalizi wa kura wa Shirika hilo wanatarajiwa kupelekwa kwa muda kuangalia kura nchini Kenya na Rwanda.

Makundi ya waangalizi hao yataangalia shughuli za kabla na baada ya Uchaguzi. Makundi haya mawili ya waangalizi wa kura yataongozwa na kamati ya wazee ya COMESA.

Amb.Dr.Simbi Mubako raia wa Zimbabwe ataliongoza kundi litakaloangalia kura nchini Kenya ambalo litawasili hapo tarehe 30 Julai 2017. Kundi la waangalizi wa kura ambalo litakwenda Rwanda linaongozwa na Bishop Mary Nkosi kutoka Malawi na mojawapo watawasili nchi Rwanda tarehe 27 Julai 2017.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Makundi hayo ya waangaizi yanatarajiwa kutoa ripoti ya kwanza kabla ya uchaguzi kumalizika na ripoti kamili kutolewa baadaye manmo siku 90.

Uchaguzi wa Kenya ambao unafanyika tarehe 8 Agosti unajiri kwa mara ya pili baada ya nchi hii kutangaza katiba mpya ya mwaka wa 2010.

Wakenya watakuwa wakichagua viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo wa rais ambako rais Uhuru Kenyatta atakuwa akiwania muhula wa pili, magavana, maseneta, mabunge, na wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa baraza la kaunti.

Uchaguzi wa Rwanda nao unakuja ukifuatia kura ya maoni  ya mwaka wa 2015 ambako wanyarwanda walichagua kubadilika kwa katiba kulikompa rais Paul Kagame uwezo wa kuwania mhula wa tatu.

COMESA imekuwa ikipeleka waangalizi wake kuangalia uchaguzi wa Rwanda tangu mwaka wa 2008 ikiwemo uchaguzi wa wabunge wa 2008 na 2013 na hata uchaguzi wa rais wa 2010.

Shirika la COMESA linawapeleka waangalizi wa kura kwenye nchi wanachama kwa jitihada za kuhimiza na kuimarisha mfumo wa demokrasia kwenye eneo hili. Shirika hilo pia linasadiki uchaguzi kuwa jambo mhimu katika kubadili maisha ya jamii na kuhakikisha misingi ya kidemokrasia inadumu

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com