kwamamaza 7

CNLG na IBUKA wapinga uamuzi wa mahakama ya Uingereza

0

Baada ya uamuzi wa mahakama ya Uingereza kutoachia kesi za wanyarwanda tano wanaoshtakiwa uhalifu katika Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 kuendeshwa na mahakama za Rwanda, mashirika mawili ikiwemo Tume ya Kupamabana na Mauaji ya Kimbari na hata shirika la Kutetea haki za manusura wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi (IBUKA) wapinga uamuzi huo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mahakama ya Uingereza ambayo ilikata uamuzi wa kesi hiyo ilidai kwamba kuwapeleka wanyarwanda hao kuendeshwa na mahakama za Rwanda kungetokea kunyimwa  uamuzi haki sawa wa mahakama. Wanyarwanda hao ni Emmanuel Nteziryayo, Vincent Bajinya, Charles Munyaneza, Charles Munyaneza, Celestin Mutabaruka na Celestin Ugirashebuja ambao wote wanashtakiwa uhalifu katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi ya mwaka 1994.

Wanaostakiwa uhalifu

 

Alipojibu haya Katibu mtendaji wa CNLG Dkt. Jean Damascene Bizimana ameiambia New Times ya Rwanda kwamba uamuzi huu ni kinyume na kanuni za kisheria na kimetoa sababu zisizo na misingi.

“Uamuzi huu haukutia maanani kwamba Mahakama ya Kimataifa ya (TPIR) na nchi mbalimbali ikiwemo Umarekani, Kanada,Norwayi , Uholanzi na Swideni zilipeleka kesi za wahalifu kama hao kuendeshwa na mahakama za Rwanda na uamuzi wa kesi zao unataolewa kwa kiwango cha kimataifa”

Aliendelea kubainisha kwamba Kanada imempeeka Leon Mugesera (ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha siku za hivi karibuni), Jean Baptiste Mugimba, Jean Bosco Iyamuremye. Umarekani nayo iliwapeleka akina Prof. Leopold Munyakazi na wengine.

TPIR nayo ikampeleka Jean Uwinkindi, Ladislas Ntaganzwa na Bernard Munyagishari.

Naphatal Ahishakiye ambaye ni katibu mtendaji wa IBUKA yeye amesema kwamba Rwanda ilizijenga ngazi zake za uongozi ikiwemo ngazi za Sheria kwa Kipindi cha miaka 23 iliyopita.

Aliongeza kwamba uamuzi huu ni wa kutenda kinume na sheria na hata kuwasaidia waliohusika na mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.