kwamamaza 7

Changamoto zitakazomkabili Rais Kagame wakati wa kuongoza UA

0

Rais wa Rwanda,Paul Kagame alianza kuongoza Umoja wa Afrika tarehe mosi,Januari 2018. Hata hivyo,wachambuzi wanaona kwamba Rais Kagame atakabiliana na changamoto kadhalika kulingana na hali iliyoko barani Afrika hasa suala la kujitegemea kwa muungano huu.

Wachambuzi wanaona kuwa haitakuwa rahisi kwake kutoa suluhisho kwa masuala ya usalama barani,migogoro ya kisiasa na ushirikiano unaoshindwa miongoni mwa nchi mbalimbali za Afrika.

Inaonekana waziwazi kuwa kazi yake ya kwanza itakuwa ya kubadili mfumo wa Umoja wa Afriak na tume yake ili kuweza kujitegemea.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwenye hotuba yake alipokuwa mjini Sham el Sheikh mwezi uliopita,Rais Kagame alisema kwamba haina budi nchi za Afrika kutoa mazingira bora ya kiuchumi.

Kinyume na hili,changamoto za ushirikiano zinajitokeza katika miungano barani kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki,sawa na SADC.

Rais Kagame alichaguliwa kuongoza Umoja wa Afrika mwezi Julai 2016 na kuchukua nafasi ya Rais wa Guinea,Apha Conde.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.