kwamamaza 7

Chama cha upinzani RNC chapiga marufuku taarifa za kusajili watakaoshambulia Rwanda

0

Kamati ya baadhi ya waliokuwa viongozi wakuu nchini Rwanda wanaounda chama cha upinzani RNC wamepiga marufuku taarifa  za chombo cha habari The Standard,nchini Kenya zisemazo kuwa kamati hii inasajili watu watakaoshambulia Rwanda.

Kupitia tangazo waziwazi, RNC imekanusha taarifa za kusajili vijana raia wa Rwanda waliyoko katika kambi za wakimbizi nchini Uganda watakaoshambulia Rwanda na kuwataka wandishi wa The Standard kurekebisha taarifa walizoandika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande mwingine taarifa za The Standard zilikuwa zikihakikisha kuwa kuna mpango wa RNC wa kusajili vijana watakaovamia Rwanda  kwa kueleza kuwa mafisa wa upelelezi wa Uganda(CMI) waliwasindikiza mafisa wa RNC kwenye kambi ya wakimbizi ya Nakivale walipohamasisha vijana  wakimbizi raia wa Rwanda waziwazi kujiunga na RNC.

Pia The Standard ilisistiza kuwa mtangazaji wake alitembelea kambi ya Nakivale kisha wakimbizi wakamuambia kuwa jambo hili lilitokea.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kamati la RNC liliundwa  na wapinzani wa serikali wa Rwanda wakiwemo Kanuni Patrick Karegeya,Dk.Theogene Rudasingwa,Jenerali Kayumba Nyamwasa.

Haya ni baada ya taarifa za baadhi ya vyombo vya habari nchini Uganda kama vile Chimpreports kutangaza kuwa kuna vita baridi kati ya Rwanda na Uganda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.