kwamamaza 7

Chama cha RNC chapiga marufuku taarifa za chombo cha habari The Standard husika na Wanyarwanda waliokamatwa

0

Chama cha Rwanda National Congress kimekanusha taarifa za chombo cha habari The Standard kilichotangaza kuwa wakimbizi 40 asili ya Rwanda waliokamatwa kwenye mpaka wa Kikagati walikuwa wakielekea nchini DR Congo ili kuhudhuria mafunzo ya kijeshi ya chama hiki.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kupitia msemaji wa RNC,Jean Paul Turayishimiye akiwa mijini Bostoni,Marekani amesema kuwa chama taarifa hizi si ukweli kwa kuwa polisi ya Uganda iliyowakamata haijatangaza kuwa hawa walikuwa Wanyarwanda wakielekea kwenye kambi za mafunzo nchini DR Congo kwa msaada wa RNC.

Jean paul Turayishimiye ametangazia VOA kuwa vyombo vya habari vilivyotangaza taarifa hizi vinadhamiria kusamabaza anachokiita ‘propaganda za serikali ya Kigali’.

Huyu amesema kuwa chama cha RNC hakina kambi za kijeshi nchini DR Congo na kuwa inabidi kungoja polisi ya Uganda itakayofafanua lengo lasafari ya wakimbizi hawa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hii si mala ya kwanza chama hiki kukanusha taarifa za chombo cha habari The Standard,hili ni baada ya kiongozi wa chama cha RNC, Jenerali Kayumba Nyamwasa kukanusha taarifa za chombo hiki zilizokuwa zikisema kwamba RNC inasajili vijana wakimbizi asili ya Rwanda kutoka kambi zao nchini Uganda ili kuwapa mafunzo ya kijeshi kwa msaada wa mafisa wa upelelezi wa Uganda(CMI) hasa kiongozi wake Brig.Jenerali,Abel Kandiho.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.