Swahili
KIMATAIFA

Chama cha RNC chabadili  mkakati wa ‘kuipaka masizi’ serikali ya Rwanda

Kuna taarifa  kwamba washiriki wa  chama cha upinzani kwa serikali ya Rwanda, Rwanda National Congress,RNC nchini Uganda wamebadili mkakati wa kuipaka masizi serikali ya Rwanda kama inavyotangazwa na chombo cha habari nchini Kenya,The Standard.

Taarifa za hiki chombo cha  habari zinasema kuwa wanachama wa RNC walikuwa na uzoefu wa kuishtaki serikali ya Rwanda ‘kuwateka nyara’  wakimbizi asili ya Rwanda wanaoishi nchini Uganda na kuwa mkakati huu ulishindwa.

The standard inaeleza kwamba mkakati mpya huu wa RNC ni kueneza habari za uongo kuwa serikali ya Rwanda inawasaidia wauaji  kuwaua viongozi wa ngazi za juu za serikali ya Uganda kwa msaada wa  maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,wanachama wa RNC hasa Rugema Kayumba, walishatki serikali ya Rwanda kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame,Luteni Joel Mutabazi ambaye alikamatwa nchini Uganda na kuhukumiwa kufungwa maisha jela na mahakama ya kijeshi nchini Rwanda.

Kwa upande wa Rwanda,kupitia msemaji wa polisi CP Theos Badege walikanusha haya madai kwa kueleza kwamba Luteni Mutabazi alikamatwa kufuatia sheria za kimataifa na  mkataba wa kutumiana wahalifu uliotiwa saini kati ya Rwanda na Uganda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com