Swahili
Home » Chama cha Jen. Kale Kayihura chalaani mashtaka ya kuwaua watu kumi nchini DR Congo
HABARI MPYA

Chama cha Jen. Kale Kayihura chalaani mashtaka ya kuwaua watu kumi nchini DR Congo

Msemaji wa  chama cha Rwanda National Congress(RNC), Jean Paul Turayishimiye amepiga marufuku mashtaka ya kwamba  kuna wanamgambo wao wanaoshiriki katika vita vya kikabila vilivyoua watu kumi.

Msemaji wa RNC, Jean Paul Kagame/ picha na Intaneti

Akizungumza na Sauti ya Marekani leo tarehe 22 Juni, Turayishimiye amehakikisha kwamba chama chao hakina wanajeshi nchini DR Congo na kuwa aliyotangazwa ni uongo mtupu.

“ Yaliyotangazwa na kiongozi wa Wanyindu ambaye hatumujui,yule si msemaji wa RNC. Haya yote ni propaganda za Rwanda,ninayojua ni kwamba  hakuna wanajeshi wa RNC  eneo la Bijombo”

Pia amelaani madai ya wakazi wa Bojombo wanaosema kuwa wanawaona wanajeshi wa Kayumba Nyamwasa.

“  Kuna makundi mengi ya wanamgambo huko, hawa wakazi hawawezi kutambua hawa ni wa RNC, siyo rahisi  kutambua kwani kuna Wafulero,Wanyindu, Warundi…” amesema

“ Hatukuwahi kutangaza kwamba kuna wanajeshi wetu nchini DR Congo, hizi ni taarifa za vyombo vya habari”

Chama cha RNC kimefunguka haya baada ya viongozi wa Mmoja mwa viongozi wa eneo la Minembwe Gad Mukiza kuhakikisha hivi vita vimesababisha watu wengi kukimbilia Minembwe.

Pia kiongozi makamu wa Wanyindu, Pierrot Baroka alitangazia Sauti ya Marekani kuwa Wanyamulenge wanaungwa mkono na wanamgambo kutoka Rwanda wanaosema kuwa hawa ni Jen. Kayumba Faustin Nyamwasa.

Viongozi wa ngazi za chini wamehakikisha wengi  wameisha kimbia hasa maeneo ya Rubarati, Mbundamo, Masango, Kanogo, Rubibi, Mugogo, Gatoki na Maheta.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com