Home HABARI MPYA Burundi: Mungu aliye waumba warundi anawapenda-Rais Nkurunziza
HABARI MPYA - November 10, 2016

Burundi: Mungu aliye waumba warundi anawapenda-Rais Nkurunziza

Kwenye maombi ya siku moja yenye lengo la kuwakutanisha viongozi wote wa Burundi, hapo rais Nkurunzi alisema kwamba tangu mwaka 2015 Mungu aliwatendea makuu ijapo kuwa kuna wale hawakufurahia, Mungu aliwaumba akiwapenda.

Rais alisema ndio walipatwa na matatizo, Mungu hatishwi na matatizo, hayo yote ni kwa kuwa watu waweze kumufuata Mungu na kumutii, hata watu wawakatae, wanachokiamini ni kuwa Mungu yupo pamoja nao.

[ad id=”101″]

Aliendelea kusema kwamba anashukuru Mungu kwa yote amewatendea, kupitia nguvu za maombi Mungu anafanya makuu yenye binadamu hawezi kufanya.

Kwa hayo rais amesema kwamba wale ambao wana mipango michafu kwa ajili ya Burundi wakome, eti Mungu aliumba warundi tena anawapenda na huwatendea mema bila shaka.

Denise Nkurunziza, mke wa rais amesema kwamba kupitia maombi; Mungu anawafunulia mengi hata wale waliohitaji kumuondoa mume wake madarakani walikua wakijua yatayofanyika.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.