Mnyarwanda Goreth Kayiranga ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya usafirishaji,Volcano LTD alikamatwa  wilayani Muyinga,kaskazini mashariki nchini Burundi kwa kutuhumiwa kuwa mpelelezi wa Rwanda.

Goreth Kayiranga alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa Burundi alipokuwa kazini kwenye mpaka wa Burundi na Tanzaniya eneo la Kobero.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za ‘Collectif SOS Médias Burundi’ zinasema kuwa Kayiranga anashtakiwa kutumwa na Rwanda kuwa mpelelezi wa Rwanda.

Wafanyakazi wenzake wemetangazia Bwiza.com kuwa wanajaribu kujua chanzo cha jambo hili na kuwa hawajapata habari kamili.

Afisa wa kampuni hii, Agaba Andrew amesisitiza kuwa watafanya juu chini kujua  chanzo cha jambo hili na kuwa kuna imaani kwamba Goreth atachiwa huru leo kulingana na mazungumzo yaliyokuwepo kati yao na polisi ya Burundi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina