kwamamaza 7

Burundi yaweka wazi kuna yanayofanyika kisiri kuboresha ushirikiano na Rwanda

0

Waziri wa Mambo ya Nje nchini Burundi, Ezechiel Niyibigira jumanne wiki hii alitangaza kuna mipango ya kisiri inayoendela kwa kuboresha ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi na Ubegiji kwa kutoa suluhisho za masuala ya kisiasa yaliyojitokeza tangu mwaka 2015.

Waziri Niyibigira aliweka wazi haya kwenye  mkutano uliotokea kati yake na mabalozi wan chi nyingine nchini Burundi pamoja na mashirika ya kimataifa.

kwa mujibu wa taarifa za Sauti ya Marekani mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwajulisha hali ya mambo nchini Burundi.

Pia , Kiongozi alisema  Burundi itashiriki katika mazungumzo yatakayotokea nje ya nchi kati yake na wapinzani.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ezechiel Niyibigira

Ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi ulianza kuwa ovyo tangu mwaka 2015 ambako Burundi ilishtaki Rwanda kuwaunga mkono waliolenga kupindua utawala wa Rais Nkurunziza.

Kwa upande mwingine, Rwanda ilikanusha haya yote na kunyoshea kidole Burundi kwamba inawahudumia wale amabao wanataka kuharibu usalama wake.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.