kwamamaza 7

Burundi yatangaza itapambana na adui yeyote baada ya kudai Rwanda ilivamia anga yake

0

Serikali ya Burundi imetangaza  ingali tayari kupambana na adui yeyote baada ya kudai kwamba ndege ya jeshi la Rwanda (RDF)  ilivamia anga yake maili nne siku zilizopita.

Burundi imeweka wazi ndege hii ilionekana katika anga la Burundi tarehe 13 Julai mwaka huu mkoa wa Kayanza kama ilivyohakikishwa na Gavana wake, Anicet  Ndayizeye.

“Nataka kuwajulisha kwamba ndege ya Rwanda ilionekana katika anga letu huku wilayani Kabarore. Ilikuja na kuchunguza vituo vyetu vya jeshi na kurudi nyuma” Gavana Ndayizeye alisema Ijumaa iliyopita

Waziri wa Utawala wa nchi, Pascal Barandagiye amesema Burundi ingali tayari kupambana na yeyote anayetaka kuharibu usalama wake kama ilivyokuwa tangu zamani.

“ Warundi wangali tayari kama ilivyokuwa katika historia yao tangu zamani. Haitakuwa mala ya kwanza… nadhani kwamba mnakumbuka mwaka 2015 walioshambulia kutoka Kayanza. Siwezi kuongea mengi husika ila ninachowaambia wakazi ni kwamba tuko tahadhari” Waziri Barandagiye ametangazia Radiyo  Sauti ya Marekani

Waziri wa Utawala wa nchi, Pascal Barandagiye

Waziri Barandagiye ameongeza jambo la kufanya kuhusu hivi vitendo vya Rwanda linahusu mno jeshi la Burundi.

Pia Katibu Mkuu wa chama tawala, Evariste Ndayishimiye amesema Burundi ilishtaki Rwanda kutokana na  hivi vitendo katika miungano ya EAC na ICGLR na kuwa hawajapata jibu bado.

“ Hayo hayawezi kutufurahisha sisi Warundi”

Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi nchini Burundi haijatangaza lolote kuhusu haya.

Waziri wa Ulinzi, Kanuni Biyereke Philbert alisema usalama kwenye mipaka ungali katika hali nzuri na kutahadharisha jeshi kuhusu ulinzi wa mipaka hasa karibu na Rwanda.

Kwa upande mwingine, Rwanda haijatoa bado maelezo kuhusu haya madai ya Burundi.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.