Msemaji wa Serikali ya Burundi, Prosper Ntahorwamiye amesisitiza Rwanda ni jirani mbaya na kuwa mashambulizi nchini mwake yanatoka Rwanda.

Prosper litangaza haya kwenye mazungumzo na vyombo vya habari tarehe 19 Disemba mwaka 2018.

“  Kuna changamoto kati ya Burundi na Rwanda. Wanaishi nchini humo walioenga kupindua serikali ya Burundi. Hawakuweza kutimiza hili lakini walijaribu Mungu akaokoa.” Prosper alisema

“ Ilionekana wazi wazi kwamba wanaoshambulia Burundi wanatoka nchini Rwanda. Ndege ya Rwanda ilionekana katika anga letu bila idhini (…). Tunawambia hatutaenedelea kuandalia haya mambo bila kufanya chochote.”

Huyu Kiongozi alihakikisha kwamba masuala ya kisiasa yaliyoko kati ya Rwanda na Burundi yalimfanya Rais Nkurunziza kumtumia barua Mkurugenzi wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni.

[penci_related_posts taxonomies=”undefined” title=”Habari nyingine” background=”” border=”” thumbright=”no” number=”4″ style=”list” align=”none” displayby=”recent_posts” orderby=”random”]

Ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi ulianza kuwa mkia wa mbuzi tangu mwaka 2015.

Burundi walishtaki Rwanda kuwasaidia waliojaribu kupinuda utawala wa Rais Nkurunziza mwezi Meyi 2015.

Rwanda ililaani mashtaka yote kwa kusema haiwezi kufanya hili jambo kwa kuwa halina faida yoyote kwake.

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.