kwamamaza 7

Burundi yalaani walioshambulia Rwanda walitoka kwao

0

Serikali ya Burundi imepiga marufuku madai ya Rwanda kwamba walioshambulia wilayani Nyaruguru,kusini mwake  terehe 2 Julai 2018  na kuiba mali ya wakazi walitoka nchini humo.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Burundi, Terrence Ntahiraja ametangazia BBC kuwa  hakuna mtu kutoka Burundi aliyeshambulia Rwanda na kuwa haya madai ni uongo mtupu.

“ Hayo ni uongo, ni kudanganya. Wanakosa wa kushtaka, hakuna raia wa Burundi aliyeshambulia  Rwanda”

Akijibu kuhusu uhaba wa usalama kwenye mpaka wa Burundi na Rwanda siku hizi, Waziri Terrence amesema “ Hakuna suala kama hilo”

Waziri huyu amesema kuwa wanajeshi wa Burundi walifanya uchunguzi wa usalama eneo la Kibira kama kawaida kwani kazi yao ni kulinda usalama wa nchi.

Hata hivyo, Shilika la SOS Burundi kupitia kuta wa Facebook wa hili shilika lilieleza serikali ya Burundi ilidanganya raia wake na nchi nyingine ilipotangaza inawatafuta wanamgambo inayosema kuwa wanajificha katika msitu wa Kibira,wilayani Mabayi na Bukinanyana  tarehe 21 Juni mwaka huu.

Mmoja mwa vijana ambaye ni mkazi wa eneo hili, ametangaza  hawa wanamgambo wanaishi hukokwa miezi miwili wakiwa na vifaa vya kijeshi wanavyopatiwa na bataliyani ya 112  ya jeshi la Burundi.

Kuna taarifa kwamba viongozi wa hawa wanajeshi wa Wanyarwanda ambao Warundi wanawaita “ Interahamwe” wanaishi hotelini ya eneo la Ndora.

Kwa upande wa Rwanda, Msemaji wa Polisi nchini Rwanda, CP Theos Badege jumatatu wiki hii alihakikisha watu wenye bunduki ambao hawajajulikana kutoka Burundi kupitia Mbuga ya wanyama ya Nyungwe  walishambulia wilayani Nyaruguru, kusini mwa Rwanda.

Kwa sasa, haijaeleweka waziwazi wanatoka wapi watu wanaoshambulia Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/ Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.