kwamamaza 7

Burundi yaishtaki Rwanda kuhudhuria mipango ya kuharibu usalama wake

0

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amelitaka shilika la Kiuchumi la nchi za Afrika ya Kati (CEEAC) kupata mikakati ya kuzuia mpango wa Reynders/Soros/ Mo-Ibrahim/Katumbi-Mbemba unaoandaliwa nchini Rwanda.

Rais Nkurunziza alisisitiza kuwa huu mpango unalenga kuharibu usalama nchini Burundi na kwa eneo la maziwa makuu.

Taarifa za Burundi ABGNews imeeleza Rais Nkurunziza alimkaribisha  Makamu Katibu Mtendaji Tabu Abdallah Manirakiza na kusisitiza kwamba miradi haiwezi kutekelezwa bila usalama.

Burundi inasema kwamba Rwanda inaungana mkono na nchi nyingine kama Ufaransa, Ubelgiji, Marekani na Canada.

Hata hivyo, Rais wa Rwanda Paul Kagame alitangazia Jaune Afrique kwamba  Warundi hawana budi kutatua matatizo yao badala ya kuangalia majirani wao.

Serikali ya Burundi tangu mwaka 2015 ilinyoshea kidole Rwanda katika mashilika mbalimbali EAC, CIRGL na CEEAC kuwaunga mkono watu wanaolenga kushambulia Burundi.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.