Msemaji wa Rais Nkurunziza, Jean Claude Karerwa

Msemaji wa Rais wa Burundi, Jean Claude Karerwa ameweka wazi msimamo wa nchi yake kuhusu madai kwamba watashambulia Rwanda kabla ya Rwanda kufanya hilo.

Huyu kiongozi ametangaza hayo  wiki iliyopita akizungumza na kituo cha televisheni ya nchi kwa kueleza waziwazi  changamoto zilizoko kati ya Rwanda na Burundi.

Akijibu ikiwa watashambulia Rwanda, Karerewa amesema hilo lilitokea miaka mingi liyopitana kuwa  hawataki vita siku hizi.

“ Nimekuamabia yalitokea zamani. Tunaomba Mungu hayo kutotokea tena. Tunaomba Mungu hilo kwani vita vinaharibu tu, havijengi.”

Msemaji wa Rais Nkurunziza, Jean Claude Karerwa

Pengine Karerwa ametangaza wakishambuliwa watafanya lolote kujilinda.

“ Huwezi kukaa na kutofanya chochote unaposhambuliwa. Haina budi kupambania nchi yako,amani na usalama. Tuna kila chochote kuanzia kwa Mungu na wanadamu. Karerwa amejulisha

[penci_related_posts taxonomies=”undefined” title=”Habari nyingine” background=”” border=”” thumbright=”no” number=”4″ style=”list” align=”none” displayby=”recent_posts” orderby=”random”]

Mtangazaji alipotia mkazo kwenye suali la kushambulia Rwanda, Karerwa alisema hakuna mpango baali wangali tayali kila upande.

“ Hakuna mpango huo nchini Burundi hata katika ndoto. Kuna mpango wa kuwa tayali. Siwezi kufichua kila kitu hapa lakini tumeisha tia ulinzi wowote angani, chini na mipaka.”

Ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi ulianza kuwa mkia wa mbuzi tangu mwaka 2015.

Habari husika: https://swahili.bwiza.com/burundi-yasisitiza-wanaotushambulia-wanatoka-nchini-rwanda/

Burundi walishtaki Rwanda kuwasaidia waliojaribu kupinuda utawala wa Rais Nkurunziza mwezi Meyi 2015.

Rwanda ililaani mashtaka yote kwa kusema haiwezi kufanya hili jambo kwa kuwa halina faida yoyote kwake.

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.