kwamamaza 7

Burundi: Wanyarwanda 8 wahukumiwa kwa uchimbaji wa magodi

0

Wanyarwanda nane wanafungiwa gereza ya Ngozi, baada ya kushikwa wakichimba kolta(coltan) kinyume na sheria kwenye Kilima cha Ryamukoma kwenye wilaya ya Kabarore, mkoa wa Kayanza kaskazini mwa nchi ya Burundi.

Wanyarwanda hao ni pamoja na: Samuel Ndikuriyo, Bosco Nyandwi, Augustin Nyandwi, Jean Claude Nzeyimana, Vianney Sakubu, Ferdinand Uwizeyimana na Jean Claude Musabyimana.

Wanyarwanda hawa walishikwa mnamo siku 10 zilizopita, na wakaletwa mbele ya mahakama siku iliyofuata, muendesha mashtaka aliambia korti kwamba wanashtakiwa kuingia Burundi kwa njia isiyo halali na kuanza uchimbaji na uporaji wa magodi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Washtakiwa walikana mashtaka, bali waliomba msamaha wakidai kwamba ni njaa iliyoko nyumbani mwao iliyowasababisha kufanya hivyo kama tovuti ya Ikiriho inavyoeleza.

Baada ya kusikilizi madai yao, muendesha mashtaka aliwaombea hukumu ya kufungwa miaka 10 na kulipa faini ya milioni 100 za faranga za Burundi kila mmoja kama inavyoelezwa katika ibara ya 155 na ya 158 ya sheria inayohusu uchimbaji wa magodi na hata ibara ya 414 ya kanuni za adhabu. Mahakama baada ya kuchambua kesi iliamuru kifungo cha miaka 10 kwa kila mmoja.

Wanyarwanda hawa wanajiunga kwa wengine 11 ambao wanafungiwa gerezani Ngozi kwa mashtaka sambamba. Hawa nao walishikiliwa Kabarore wakijaribu kuvuka nchi wakiwa na tani moja na kilo 70 za Kolta.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.