kwamamaza 7

Burundi: Wakazi wababaika kwa fununu za shambulizi kutoka Rwanda

0

Raia wa Burundi karibu na mpaka wake na Rwanda wamekimbia baada ya kusikiliza fununu kwamba kuna shambulizi  kutoka Rwanda.

Wakazi wa maeneo ya  Ruziba, Wilayani Mugina na Ruhwa Wilayani Rugombo mkoa wa Cibitoke jana  wamejulisha polisi nchini humo kwamba kuna kundi la watu wenye silaha ambalo limevuka mpaka wa Rwanda kuelekea Burundi.

Kwa mujibu wa ukuta wa Twitter wa SOS Burundi, vijiji vizima vilikuwa katika hali ya fujo kutokana na hiki kisa.

Mmoja mwa hawa wakazi ambaye ni mkazi wa tarafa ya Ruce amesema” Tumeona wanajeshi wa ulinzi wa usiku wakienda kwa kasi,tumefikiri kwamba kuna watu ambao wamevuka  mto wa Ruhwa kutoka Rwanda”

Viongozi vijijini humo wameeleza  hizi taarifa ni fununu zilizosambazwa na wakazi na kuomba jeshi kuroa msaada huko karibu na mpaka.

Jeshi la Burundi limekuja tayari kupambana lakini ilikuwa ni fununu na kuwaambia wakazi kutoa habari  wakati kuna suala la usalama katika maeneo yao.

Mala nyingi Burundi  inakuwa tahadhari karibu na mpaka wa wanda  kwa kusema waliojaribu kuipindua serikali ya Nkurunziza wako nchini Rwanda.

Hata hivyo, Rwanda hukanusha haya madai kwa kusema masuala ya Burundi yanahusu raia wake wenyewe.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.