kwamamaza 7

Burundi: Sensa ya kujaza utambulisho yatia uoga wafanyakazi wa serikali

0

Fomu inayotakiwa kwa wafanyakazi wa serikali kujaza majina yao na jamii wanakotoka, kwa ombi la Seneti, imezua utata nchini Burundi. Wafanyakazi wa serikali wametakiwa kuweka majina yao, umri, jinsia, na kutaja kabila na mkoa wanakotoka kwenye fomu hiyo.

Kwa mujibu wa serikali ya Burundi, sensa hii ni kipimo kinachoruhusiwa na Katiba ili kuboresha idadi kwa wafanyakazi wa serikali kulingana na makabila yanayounda jamii ya Warundi.

Uchunguzi uliyoagizwa na Baraza la Seneti kuhusu wafanyakazi wa serikali unakwenda sambamba na sheria, Baraza la Seneti lenye majukumu ya kuchungua usawa wa kikabila katika mashirika na makampuni ya serikali, limebaini.

[ad id=”72″]

Sensa hii inawatia uoga baadhi ya wafanyakazi ambao wanahofia kwamba matokeo yake huenda yakatumika kwa ajili ya malengo fulani.

Léonce Ngendakumana, mmoja wa viongozi wa upinzani, anabaini kwamba sensa inayoendeshwa katika mazingira ya kisiasa ya sasa kuna hatari yavunje usawa wa kikabila wa nchi ya Burundi.

“CNDD-FDD (chama tawala) kilikua kikipanga kuingilia masuala ya usawa wa kikabila na kinaweza kutumia uchunguzi huu kwa kuvunja usawa huo. Hatari ya pili ni kwamba uchunguzi huu unaweza kusababisha kukwamisha uzoefu na umahiri wa watumishi wa umma,” amesema Ngendakumana.

Ngendahimana ameonya kwamba Sensa inaweza kutumika kwa kuwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi ambao tayari wamepata uzoefu katika neema ya wafanyakazi wapya, wakisema kwamba katika shirika au kampuni fulani kabila fulani linaongoza kwa watu wengi; kama huripotiwa na RFI.

[ad id=”72″]

“Zoezi hili la Kamati ya Uchunguzi ya Baraza la Seneti hailengi kufukuza kazi watu kutoka kabila fulani. Madhumuni yake ni kufanya uchunguzi ili kukosoa hatua kwa hatua kile kisichokua sawa katika usawa wa kikabila na kuhakikisha kwamba hakuna mkoa au kundi la watu fulani limetengwa kwa manufaa ya huduma za umma “, amesema Stella Budiriganya, msemaji wa rais wa Baraza la Seneti.

Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha, unaounda Katiba ya Burundi, unaeleza kwamba idadi ya vikosi vya usalama inapaswa kuundwa na wajumbe 50% kutoka kabila la Watutsi na 50% ya wajumbe kutoka kabila la Wahutu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.