kwamamaza 7

Burundi: Maafisa wa polisi wajeruhiwa katika shambulizi kali

0

Washambulizi wasiojulikana walivamia jengo la hoteli ya Phoenicia mkoani Bururi, nchini Burundi katika usiku wa Alhamisi na watu 7 wamejeruhiwa; miongoni mwao kuna maafisa 3 wa polisi.

Msemaji wa polisi nchini Burundi, Pierre Nkurikiye alisema kwamba shambulizi lilipatikana usiku wa manane; wakati washambulizi wawili waliingia ndani ya hoteli na kurusha mfululizo wa lisasi.

Miongoni mwa majeruhi, kuna kiongozi makamu wa polisi mkoani Bururi; kiongozi wa upelelezi katika Bururi na mlinzi wake.

[ad id=”72″]

Watuhumiwa 20 wametiwa mbaroni baada ya tukio hii ambayo imefikiriwa kama shambulizi la kigaidi.

Hali imeendelea kuwa mbaya tangu mwaka uliopita wakati rais Nkurunziza alionyesha jitihada za kugombea urais kwa muhura wa tatu.  katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bujumbura na sehemu nyingine kulisikiwa mashambulizi tofauti, ijapokuwa siku hizi kuna utulivu kulinganisha na siku zilizopita.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.