kwamamaza 7

Burundi: Kundi la Majambazi likiwemo anayetumikia Rwanda wakamatwa hotelini

0

Kundi la Majambazi saba  likiwemo anayetuhumiwa kutumikia Rwanda wamekamatwa hotelini kwa jina la ‘Maison Jaune’ tarehe tatu Septemba 2018.

Polisi nchini Burundi  imehakikisha mmoja wao, Pontien Baracambariza  ni jambazi hodari ambaye anatumia bunduki kuiba nchini Rwanda na Kenya.

Inasemekana huyu alimuiba bunduki polisi wa Kituo cha polisi Wilayani  Mwumba,Mkoani Ngozi.

Wengine waliokamatwa ni Bigirimana Eugene, Irambona Joseph, Ntihabose Piyo, Nimbona Jimmy, Ndayiragije Jean Claude ndetse na Ndizeye Reverien.

Taarifa za UBM News ni kwamba hawa wanakubali kuwa na hatia baada ya kupatikana wakiwa na bunduki moja na grunedi na kuwa waliiba sehemu nyingi kijijini.

Polisi ya Burundi imesema watuhumiwa watasimama kizimbani juu ya uhalifu wao.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.