Kiongozi wa ngazi za chini Mkoa wa Cibitoke Wilayani Mabayi, Messiah Ntunzwenabo amekamatwa juu ya kuuza silaha kwa kundi la watu wanaotumia lugha ya Kinyarwanda.

Kwa mujibu wa SOS Media Burundi, Ntunzwenabo na dereva wake walikamtwa Alhamisi wiki iliyopita wakimiliki bunduki tatu za aina ya AKA47.

Taarifa hizi zinaendelea kusema hawa walikuwa wakifanyia hii biashara yake katika msitu wa Kibira.

Viongozi wegine wamesisitiza waliona watu ambao hawakuwajua katika hili eneo.

“ Tuliona watu wengi wakiendelea na shughuli zao katika hili eneo.” Kiongozi mmoja amesema.

Kwa upande mwingine hizi taarifa hazielezi hili kundi la watu wenye silaha linaishi wapi.

Gavana wa Mkoa wa Cibitoke amehakikisha hizi taarifa.

Hili ni baada ya Gavana wa Mkoa wa Cibitoke kumfukuza kazini kiongozi  wa Kijiji mwingine kwa majina ya Wilson Bakara kwa kutuhumiwa uhusiano na kuungana mkono  na wanamgambo kwa kuchimba migodi msituni Kibira.

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.