kwamamaza 7

Boti linahofia kuzama kati ziwa Tanganyika na 6 kupoteza maisha

0

Watu sita wanahofiwa kufa maji na shehena ya mizigo yenye bidhaa mbalimbali inasadikiwa kuzama ndani ya ziwa Tanganyika baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupotea kwa zaidi ya siku 10 sasa.

Tetesi za kupotea kwa boti hiyo zimezagaa sehemu mbalimbali mkoani Kigoma na Polisi mkoani Kigoma imethibitisha ajali hiyo na juhudi za kuitafuta zinaendelea.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema boti hiyo iliondoka Januari 21, mwaka huu katika bandari ya Kibirizi kwenda Kalemie katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na hadi leo haijafika ilipokuwa ikielekea.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kamanda Mtui alisema boti hiyo ijulikanayo kwa jina la Mv.Ngendo ya Buchuma, mali ya Mussa Hamisi ambaye ni mkazi wa Ujiji mjini Kigoma, ilikuwa imebeba shehena ya vitunguu na ngano ambavyo vilikuwa vikipelekwa Kalemie ikiwa na watu sita wakiwemo wafanyakazi wa boti hiyo.

Kwa mara ya mwisho, Kamanda Mtui alisema boti hiyo ilionekana upande wa DRC na kwamba hadi sasa haijulikana boti hiyo imekumbwa na nini na iko wapi.

“Kwa sasa polisi wanamaji kwa kushirikiana na chama cha wamiliki wa maboti Mkoa wa Kigoma tunaendelea na msako wa boti hiyo sambamba na kutoa taarifa kwa mamlaka za Mji wa Kalemie nchini DRC kuhusiana na kupotea kwa boti,” alieleza Kamanda Mtui.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.