Home BIASHARA Biashara ya Uchukuzi yarahisishwa kwa kufuta Kodi
BIASHARA - HABARI MPYA - SIASA - June 15, 2017

Biashara ya Uchukuzi yarahisishwa kwa kufuta Kodi

Wafanyabiashara wa kuagiza magari ya uchukuzi wa mizigo na abiria pamoja na wamilki wa mashirika ya uchukuzi, wana furaha kubwa baada ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Uchumi( MINECOFIN) Kufuta kodi ama kupunguza kwa baadhi ya magari.

Wafanyabiashara hawa wanasema kwamba hatua hii itafanya bei ya magari haya kupunguka na kuongezeka hadi watu waone bora kusafiri na magari ya umma na hii kufanya msululo wa magari jijini Kigali kupunguka.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi, Claver Gatete alipokuwa akifafanua mpango wa bajeti wa 2017/18 mbele ya bunge alisema kwamba mashine za trakta za kutengeneza barabara zitalipa kodi 0% kutoka 10% ya awali.

Magari ya mizigo yenye uwezo wa kuchukua kati ya tani 5 na 20 atalipa kodi ya 10% kutoka 20% ya awali. Magari yenye uwezo wa kuchukuwa zaidi ya tani 20 atalipa kodi ya 0% kulingana na 25% ya awali..

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mabasi yenye uwezo wa kuchukua watu kati ya 25 na 50 atalipa 10% kulingana na 25% ya awali huku mabasi yenye uwezo wa kuchukuwa zaidi ya watu hao akilipa bure kulingana na 25% ya awali.

Wanaofanya biashara hiyo wanaona kwamba hatua hiyo ya kufuta na kupunguza kodi kwa magari hayo itasaidia bei yake kupunguza kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwa rahisi kwa watakaotaka kununua magari hayo.

Baadhi ya bidhaa kutoka nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki nazo zilipunguziwa ushuru kwa ajili ya mfumo wa kuendeleza viwanda vya ndani ya nchi kwa mjibu wa Wizara ya Fedha na Mipango ya Uchumi. Bidhaa hizo ni kama mchele, sukari na ngano.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.