Swahili
Home » Biashara ya Kuvuka mpaka kuimarika kufuatia masoko yanayokaribia kukamilika.
BIASHARA

Biashara ya Kuvuka mpaka kuimarika kufuatia masoko yanayokaribia kukamilika.

Soko la Cyanika kwenye hatua za mwisho

Jududi za kukamilisha ujenzi wa masoko manne ya kuvuka mpaka zinafanyika na inategemewa kwamba mojawapo yatazinduliwa baadaye mwezi huu.

Masoko ambayo anajengwa ni pamoja na soko la Cyanika liloko wilaya ya Burera karibu na mpaka wa Uganda, la Karongi na la Rusizi I yaliyoko karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yote yakiwa kwenye hatua za mwisho kukamilishwa.

Kulingana na habari alizoipa The New Times waziri François Kanimba  wa Biashara, viwanda na Shughuli za EAC zinasema kwamba na hata soko la Rubavu liko kwenye hatua ya 70% na inatarajiwa kuwa litakamilika mnamo mwisho wa mwaka huu.

Wazo la kujenga masoko ya aina hii kama anavyosema waziri Kanimba limekuja baada ya serikali kuona kwamba wafanyibiashara ya kuvuka mpaka wamekuwa wakikumbwa na matatizo mengi ambayo ingeifanya biashara yao kutokwenda vizuri na ikatokea kwamba wanaamua kufanya biashara haramu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“tunapanga kuzindua masoko ya Cyanika na Karongi baadaye mwezi huu wa (Julai), sehemu ya soko la la Rusizi I inaweza kuanza kutumika ingawa tunapanga kuiongezea nafasi kwa ajili ya matumizi na wafanyibiashara wengi,” Amesema waziri Kanimba.

 Kunajengwa masoko mengi ikiwa kuna mpango wa kueneza masoko ya aina hii kwenye mipaka yote ya nchi kwa ajili ya kurahisisha wakazi wa maeneo ya mipaka na wafanyibiashara ya hapo. Masoko mengine ambayo yanajengwa ni mfano wa soko la Rugari liloko wilaya ya Nyamsheke na litagharimu takriban 700 milioni za faranga za Rwanda.

Mengine ambayo yanatarajiwa kujengwa ni la Kagitumba karibu na mpaka wa Rwanda na Uganda na la Rusumo karibu na mpaka wa Rwanda na Tanzania na ujenzi wake utaunganishwa na mradi mkubwa wa kujenga barabara kubwa kutoka Kagitumba hadi Rusumo.

Masoko kama ya mipaka ya Nemba na Gatuna yatajengwa kulingana na jinsi uwezo wa kifedha utakavyopatikana.

Soko la Cyanika na la Karongi yatagharimu bilioni 1.5 za faranga za Rwanda kila moja, la Rubavu bilioni 2.6 na la Rusizi bilioni 1.2 ingawa serikali inapanga kuwekeza bilioni 1.9 kwa kuliongezea uwezo.

Waendeshaji shughuli za kibnafsi walifurahia hatua hii ya kujenga masoko kwenye mipaka kwa kusema yatarahisisha biashara hiyo na kuleta manufaa mengi.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com