kwamamaza 7

Barua aliyoandikiwa muathiriwa wa mauaji ya kimbali

0

Mtangazaji wa BBC, Venuste  Nshimiyimana amemuandikia barua muathiriwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994,Veronica Uwimana na kusisitiza mataifa hayakusaidia Rwanda kujikinga mabaya haya.

Veronica Uwimana ambaye ni muathiriwa wa mauaji ya kimbali dhidhi ya Tutsi mwaka 1994/Hisani

Katika barua yake, Nshimiyimana ameandika :

Ndugu mpenzi Veronica Uwimana,

Hii ni sikuu kubwa maishani mwako na kwa wengi kwa asili ya Tutsi waliouawa kiunyama mwaka 1994.

Nakufikiria kwa kuwa nakujua,najua maumivu yako na jitihada zako za kujijenga,upendo wako kwa wanao na kwa wale wanaouhitaji.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakati huu wa maadhimisho nawakumbuka wengi niliokosa kule Eto Kicukiro nilikokimbilia tarehe 7 Aprili 1994.Nakumbuka nilipotaka mataifa kutoa msaada.Nitwakumbuka milele.

Venuste Nshimiyimana aliyemuandikia Veronica Uwimana

Umoja wa Mataifa hasa nchi zilizotuma wanajeshi nchini Rwanda kama vile Ufaransa,Italy,Ubelgiji kwa kunusuru raia wake na kuacha Wanyarwanda wakiuawa pamoja na wengine waliokuwa kwenye misheni ya YUNA ambao hawakunusuru Watutsi, hawana budi kuomba msamaha na kulipa fidia.

Nakumbuka kila siku tuliyoshuhudia.Kilichonifanya kunusurika, kinanifanya nipige mayowe nikiwa kwenye mikutano ya kimataifa kwa kukumbusha kulipa fidia waliokataa kuwanusuru waliokuwa Eto Kicukiro.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakati huu,nakumbuka wathiriwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi.Nawatakia  heri na fanaka kwa Mola  wanafamila wenu waliofariki.Kunusurika kwenu ni neema ya Mungu.Muendelee kijijenga na kwa kujenga Rwanda.

Nakuandikia hii barua kukutia nguvu.Usikate tamaa.Nitakusaidia mauaji ya kimbali yasitokee tena.Nashukuru Mola kwa kuwakuta watu kama wewe wenye upendo na maadili.Waliokufa wangali hai kwani waliacha wengine watakaosaidia Rwanda kukaa imala.

Nduguyo, Venuste Nshimiyimana

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.