Swahili
Home » Barafinda asisitiza kwamba serikali haikutatua vilivyo tatizo la watoto wa mitaani
HABARI MPYA SIASA

Barafinda asisitiza kwamba serikali haikutatua vilivyo tatizo la watoto wa mitaani

Aliyekuwa akitaka kuwania urais,Barafinda Ssekikubo Fred ametangaza kuwa namna ya serikali kwa kutatua tatizo la watoto wa mtaani haitafua dafu kwani haikutia mkazo kwenye asili ya tatizo hili.

Bw Barafinda Ssekikubo Fred

Kupitia mazungumzo na Flash Fm,Barafinda ametumia takwimu za watoto wanaokuenda kufundishwa kule kisiwa Iwawa na kueleza kwamba matokeo yalikosekana.

Takwimu zinaonyesha kuwa watoto 107 walirudi kule, 225 hawana nyumbani kwao, 247 ni yatima na wengine 9 hawajui kwao.

Waliomaliza mafunzo yao kule Iwawa

Kwa hiyo,anapendekeza kwamba serikali ingewajengea nyumba za makazi yao na ile ya kufanyia kazi zao mbalimbali walizojifunza kule.

Vifaa vinavyoundwa na wanafunzi kule Iwawa

Pamoja na hayo,Waziri wa vijana,Rosemary Mbabazi kwenye sherehe ya kutoa vieti kwa watoto waliomaliza mafunzo ameleza kwamba serikali itawasaidia wakati wa miezi sita ili waweze kujitunza.

Waziri wa vijana,Rose mary Mbabazi akitoa vifaa kwa mwanafunzi kule Iwawa(All photos:Umuseke)

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com