kwamamaza 7

Balozi wa Rwanda nchini Uganda aeleza kuna “magaidi” wanaolenga Rwanda

0

Balozi wa Rwanda nchini Uganda, Rtd. Meja Jenerali Frank Mugambage ametangaza kuna “magaidi” wanaolenga kushambulia Rwanda ambao wanafanyia operesheni zao nchini Uganda.

Balozi Mugambage amefunguka haya jumatano wiki hii wakati wa kusherekea sikukuu ya 24 ya kuikomboa Rwanda.

“ Kuna magaidi fulani wanaolenga Rwanda” Balozi Mugambage amesema

Mugambage amesisitiza Uganda imeshindwa kufanya upelelezi husika na hili jambo ambalo ni kizuizi kwa usalama wa Rwanda.

“ Kushindwa kupeleleza haya mambo yanayojitokeza kwenu (Uganda) na yanahusika na magaidi ni suala la linaloudhi sana Rwanda” ameongeza

“ Haya ni masuala ambayo yanazungumziwa kupitia njia za kidiplomasia” amedai

Balozi Mugambage amesema  haya wakati ambapo ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Uganda ungali katika hali isiyo nzuri tangu mwaka 2017.

Rwanda  inashtaki Uganda kuwahudhumia watu wanaolenga kushambulia usalama wake wakiwemo Jen. Kayumba Nyamwasa.

Kwa upande mwingine, Uganda inashtaki  Rwanda upelelezi na kuwateka nyara wakimbizi asili ya Rwanda.

Hata hivyo, pande zote mbili hupiga marufuku haya madai ya upande mwingine.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.