Swahili
HABARI MPYA SIASA

Balozi wa Marekani awakuta wanaotaka kuwa wagombea urais wa Rwanda

Erica Barks-Ruggle, Balozi wa Marekani nchini Rwanda, baada yake na mabalozi wengine kutoka nchi za magharibi kuwa na mazungumzo na maafisa wa Tume ya Uchaguzi, amewakuta wagombea urais.

Mazungumzo ya mabalozi hao yalikuwa kuhusu maandalizi ya kura, na umuhimu wa Uchaguzi huru na tulivu ulipewa muda mwingi. Baadaye, balozi Erica Barks-Ruggle, alisema kuwa ana mpango wa kuwakuta wagombea wengine na kuzungumza nao kuhusu shughuli zao za kampeni na hata sera zao kuhusu wakati ujao wa Rwanda

Baada ya Mazungumzo, na maafisa wa Tume ya Uchaguzi yalitangazwa kuwa yalikuwa mazuri, ndipo alipowakuta wanaotaka kuwan wagombea urais katika uchaguzi utakapigwa hapo mwezi Agosti. Miongoni mwao ni Dkt. Frank Habineza atakaye wania kwa tiketi ya chama chake Green, na wagombea wengine huru kama Diane Shima Rwigara ambaye ni mgombea kike na Gilbert Mwenedata.

Tarehe 27 Juni ndipo tume ya Uchaguzi ya Rwanda ilipowatangaza wagombea wa 2 kuwa walikwisha idhinishwa na makamishna wa tume hiyo. Dkt. Frank Habineza ndie pekee aliyeidhinishwa Miongoni mwa wale aliowakuta balozi Erica Barks-Ruggle.

Uchaguzi utaanza tarehe 3 kwa wakaazi wa Diaspora na tarehe 4 ndani ya nchi. Wagombea rasmi wanatarajiwa kutangazwa tarehe 7 wakati tarehe 14 ni mwanzo wa kampeni kwa wagombea watakaokuwa wameidhinishwa na Tume ya Uchaguzi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com