kwamamaza 7

Baada ya mashine ya kutibu kansa kwa raia wa Rwanda na Uganda kufa, nyingine imenunuliwa

0

Mashine iliyokuwa ikiwatibu raia wa Rwanda na Uganda katika hospitali Mulago ambayo ni bingwa kwa kutibu ugonjwa huu ilikufa mwaka 2016 lakini nyingine imeisha nunuliwa na kuletwa mjini Kampala,Uganda .

Mashine mpya ya kutibu kansa.

Hizi ni habari amabazo wengi wamepokea kwa mikono miwili baada ya kutimiza mwaka mzima bila huduma za kutibiwa kansa kwa kuwa wengi mwa watu wa Afrika mashariki kama vile Rwanda,Uganda,Sudani Kusini wanataegemea mashine hii. Matangazo ya Bwiza.com kutoka The Monitor yanasema kwamba ukosefu wa mashine hii ulikuwa tatizo kubwa sana kwa wagonjwa wa kansa.

Mashine hii  ilinunuliwa Jamhuri ya Czech,barani uraya kwa bei ya shilingi za Uganda 2.7 ni kumaanisha miliyoni 640  fedha za Rwanda.Mashine hii imechukuwa nafasi ya ile iliyokufa Cobalt 60 radiotherapy Uganda iliyopokea kutoka Uchina kama zawadi mwaka 1995.Cobalt ilikufa kwa ajili ya kuharibika na kukarabatiwa mala nyingi na kushindwa kazi tarehe 27 Machi 2016 na watu 2000 walikosa huduma na wengi kuaga dunia.

Mashine ya kutibu kansa Cobalt 60 iliyokufa mwaka 2016.

Walioponea chupuchupu walishauriwa kwenda Nairobi nchini Kenya na wengine kubadilisha namna ya kutibiwa ugonjwa huu.Habari hizi zimejulikana popote baada ya kiongozi wa taasisi ya kulinda kansa nchini Uganda,Dkt Jackson Orem,kutangaza jambo hili akisema kwamba mashine  ingali mahali fulani mjini Kampala na kueleza”Mashine ingali mjini Kampala,vipande vyake tuatapata jumma tano hii na baada ya mwezi mmjoja itakuwa tayari kufanya kazi”.

Mashine iliyokufa ilikuwa ikifanya kazi kwa kutumia mionzi ya jua(radiotherapy) na kuwa uwezo wa kutibu watu 44,000 mwaka mmoja kutoka nchi jirani za Uganda.Mashine hii ni umuhimu sana kwa kuwa 3/4 ya watu wenye ugonjwa wa kansa ni lazima kutibiwa kwa kutumia mashine hii.Mashine hii mpya hutumiwa kwa kuchoma sehemu yenye kansa mwilini,pia hutibu aina nyingi za kansa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.