Swahili
Home » Baada ya maamzi ya serikali wanahabari wa Kiswahili wameunda chama
HABARI

Baada ya maamzi ya serikali wanahabari wa Kiswahili wameunda chama

Serikali ya Rwanda imekubali kuwa Lugha ya Kiswahili ni ya nne katika lugha rasmi (official language),ambazo hukubaliwa Rwanda, kwa hayo wanahabari wa Lugha ya kiswahili wameunda chama chao na wakakiita jina la WAKIRWA.

WAKIRWA (Wanahabari wa Kiswahili Rwanda) wakiwa na lengo linalosema hivi: “Kutokana na sera ya Rwanda na umoja wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki; Uhamasishaji, Ukuzaji, Uendelezaji wa lugha ya Kiswahili kwa jamii ya Wanyarwanda na Afrika ya Mashariki kwa ujumla, na kuidhinisha kiswahili kama lugha rasmi ya nne Rwanda. Tunahitaji tupate nafasi katika Afrika ya Mashariki, kupata hadhi yetu kama wanyarwada katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki”.

Mwanachama ni mwanahabari yeyote anayezungumza Kiswahili, kukipenda na yuko tayari kukiendeleza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wanachama wa WAKIRWA walichagua watakao waongoza kwa muda wa miaka tatu, na ni hawa wafuatawo.

  1. Mwenye kiti: Sylvanus Karemera
  2. Makamu mwenye kiti: Nshimyumukiza Janvier ‘Popote’
  3. Katibu: Aimant Kwizera
  4. Katibu mwenezi: Professa Malonga Pacifique
  5. Muweka hazina: Edith Nibakwe
  6. Washauri (2): Gonzaga Muganwa pamoja na Jean Louis Kagahe.
  7. Mwakilishi wa waandishi wa habari: René Anthère Rwanyange
  8. Mwakilishi wa watangazaji wa habari: Tidjarat Kabendera

 

Sylvanus Karemera aliye chaguliwa kama mwenye kitu alisema yupo tayari kwa kuendeleza Kiswahili na kujulikanisha usamini wake Rwanda, ameomba wanahabari ambao husema Kiswahili kuzingatia bahati waliopewa na serikali kwa kukubali iwe Lugha rasmi Rwanda.

Sylvanus Karemera amehamasisha ili kufanya haraka kwa kuunda sheria za chama na aliomba viongozi wa utangazaji habari na wanahabari wa Kiswahili kutiliya mkazo wa usamini wa lugha ya Kiswahili na kusaidia wanyarwanda kupata suluhisho ya kujua Kiswahili jinsi nchi iko moja wa nchi za jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com