kwamamaza 7

Baada ya kutua Rwanda usiku wa leo “Danger man ameanza mazoezi na kikosi cha Rayon Sports”

0

Olivier Karekezi ambaye anaitwa “Danger Man” kwa jina la utani ameongoza mazoezi na timu ya Rayon Sports ambayo yalikuwa ya  nguvu na ambayo alidumu masaa mawili.

 Olivier Karekezi kocha mpya wa mabingwa wa Rwanda Rayon Sports alitua kwenye uwanja wa Ndege wa Kanombe mnamo saa nane za usiku na alikuwa anangojea na mashabi wa timu ya Rayon Sports wengi.

Karekezi akiwa mazoezi na kikosi chake

Karekezi alipowasili kwenye uwanja wa ndege aliwaambia kwamba waandishi wa habari kwamba amekwisha saini mkataba wa miaka miwili na timu ya Rayon Sports na kwamba lengo lake ni kuisadia timu hiyo kufanya vizuri ikiwemo kushinda mataji zaidi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Karekezi Olivier mwenye umri wa miaka 34 anakuja Rwanda alipokuwa akifanya kazi kama kocha wa vijana wa umri chini ya miaka 17 na aliibuka mshindi wa taji la kocha wa vijana la mwaka nchini Sweden. Kwa hivi amehamia Rwanda na familia yake yote.

Atakuwa akisaidiwa na Ndikumana Hamad (Katauti) na Nkunzingoma Ramadhan ambao wote walikuwa pamoja kwenye kikosi cha Amavubi kilichofuzu tiketi ya Kombe la AFCON ya mwaka 2004.

Karekezi alikuwa mchezaji mahili wa timu ya Amavubi na ndiye aliyeshinda mabao mengi zaidi. Karekezi ana cheti cha Kiwango A cha UEFA na amekuwa akifunza timu ya vijana nchini Sweden.

Katika kazi yake alichezea timu kama APR FC, Helsingborgs IF, Hamarkameratene ,Osters IF, CA Bizertin ,Trelleborgs FF, Raa IF ambayo ndio timu ya mwisho aliyoichezea.

 yeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.