Je, unafikiri nini kwamba baada ya kifo kuna nini?

Unajua watu wengi, wamekufa.Unafikiri kwamba sasa wanaishi maisha gani? Au, Je, kuna maisha baada ya kifo? Watu wengine wanasema: “wamekwisha kufa, basi. Hakuna maisha baada ya kifo.”

Na watu wengine wanasema, kwamba roho yao hukaa pamoja nasi.

Je, ni kweli? Siyo kweli. Biblia inasema, kwamba hawapo pamoja nasi.

Unajua pia, kwamba wewe utakufa siku moja. Utaondoka kutoka duniani na utakwenda mbele ya Mungu. Labda umefikiri mambo mengi kuhusu kifo.

Tunajua kwamba, baada ya kifo kuna maisha. Biblia inasema hivi. Roho ya Mungu anayekaa ndani yetu anasema, kwamba maisha hayakomi katika mauti bali yanaendelea.

Yataendelea kwa muda gani? Siyo siku moja tu. Siyo mwaka moja tu. Wala siyo miaka milioni tu. Lakini yataendelea hata milele na milele. Maisha ya milele hayaishi kamwe. Ni ngumu kufahamu maisha ya milele. Hapa duniani mambo yote yanaisha. Lakini katika umilele hakuna mwisho.

  1. MTU ANAPOKUFA MAMBO YANATOKEA?

Biblia inasema: [Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.] (MWA 2:7)

Mungu alimfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, yaani kwa mavumbi ya udongo. Mavumbi na ardhi toka duniani. Na alimpulizia puani pumzi ya uhai. Pumzi ya uhai ni kutoka Mbinguni. Na hivi kwetu sisi kuna sehemu ya dunia na sehemu ya Mbingu.

Biblia inaendelea: [Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.] (MHU 12:7)

Mtu anapokufa maiti huzikwa ardhini. Maiti itakuwa mavumbi upesi. Nayo mavumbi yanarudia nchi tena kama yalivyokuwa.

Mungu alipoumba mtu akampulizia puani pumzi yake. Mtu anapokufa, roho yake inaondoka. Na roho yake inarudi kwa Mungu. Biblia inasema katika Waraka wa Waebrania 9:27: [Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;] (EBR 9:27)

Kwanza mtu anakufa na baada ya kufa kuna hukumu.

Hukumu itakuwa lini na wapi? Biblia inasema hukumu kubwa itakuwa hukumu ya mwisho na itakuwa Mbele ya kiti cha enzi kikubwa na cheupe. Hukumu haipo karibu na mauti, lakini itakuwa baada ya muda mrefu. Kabla ya hukumu kubwa kutokea mambo mengi makubwa yatatokea kabla ya mwisho wa dunia. Baada ya hizi ni hukumu ya mwisho. Lakini kati ya kifo na hukumu kubwa ya mwisho kuna nini? Na baada ya hukumu ya mwisho kuna nini?

Baada ya hukumu ya mwisho watu wengine watakwenda Mbinguni na watu wote ambao majina yao hayajaonekana wameandikwa katika kitabu cha uzima, watatupwa katika ziwa la moto.

Leo tunasoma kwamba kati ya mauti na hukumu ya mwisho kuna nini.

Tunajua kwamba watu wote watakufa. Waliookoka nao watakufa. Wasiookoka, watakufa pia. Katika kifo maiti inazikwa kaburini lakini roho inarudi kwa Mungu.

Kuna nini baada ya kifo? Kuna uzuri au ubaya? Je, kuna mahali pa waliopata wokovu na pa wasiopata wokovu pia? Au, je, watakwenda wote mahali pa sawasawa kungoja hukumu?

Watu wengi wanasema kwamba sisi hatuwezi kujua baada ya kifo kuna nini. Wanasema kwamba hapana mtu hajafika kutusimulia baada ya kifo kuna nini. Siyo kweli. Yesu amefika na ametusimulia. Kwa sababu yeye ni Muumba anajua ameumba nini. Watu wengi wamefufuka na wamesimulia wameona nini baada ya mauti. Roho Mtakatifu ameandika katika Biblia,  baada ya kifo kuna nini na anajua kweli. Kwa sababu tunataka kujua pia, tusome Biblia.

  1. YESU ALIONA MTU TAJIRI NA MTU MASKINI WALIKUFA

[Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na Manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.]  (LK 16:19-31)

Yesu alipoambia mfano Biblia inasema kwamba walikuwa mfano. Lakini hadithi hii haikuwa mfano. Hii ni kweli yalitokea. Yesu aliona jinsi mtu tajiri alivyofika Kuzimu na pia jinsi Lazaro alivyochukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu.

Tunaposoma kisa hiki tunaona kwamba baada ya kifo Lazaro na tajiri walijuana. Walipokuwa hapa duniani walijuana na walijuana pia baada ya kifo. Yaani walikumbuka mambo yalivyokuwa duniani. Walikuwa katika roho, bila mwili, kama walivyokuwa hapa duniani. Walikuwa na akili, kumbukumbu, usemi na maono. Walisikia maumivu na faraja. Tajiri alisikia maumivu na Lazaro furaha na faraja. Walikumbuka maisha yao duniani. Lazaro alikuwa aaminiye. Tajiri hakuna.

Baada ya mauti kunakuwa sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni kifua cha Ibrahimu na ya pili ni kuzimu. Kifua cha Ibrahimu kuna majina mengine pia.

[Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.]  (2KOR 12:1-4)

Paulo alikuwa mahali palepale kama Lazaro. Tulisoma, kwamba Paulo alitumia mahali palepale majina mawili:  Mbingu ya tatu na Peponi. Alipazuru tu. Hakujua kwamba alikuwa na maono tu au alikwenda katika mwili wake Peponi yaani Mbingu ya tatu. Sasa tumekuta majina matatu: Kifua cha Ibrahimu. Mbingu ya tatu. Peponi.

Watu wanatumia pia jina: Paradiso. Katika Biblia ya Kiswahili halipo neno: Paradiso, bali Peponi. Watu wengi hutumia Paradiso. Biblia inatumia Peponi (au Mbinguni au Bustani) Ninaomba ruhusa kutumia jina: Peponi. Biblia inatumia jina Peponi zaidi kuliko Kifua cha Ibrahimu au Mbingu ya tatu.

Peponi ni mahali pazuri sana. Paulo alipopazuru, Lazaro alikaa huko.  Mtu tajiri alikuwa mahali pengine, jina la pale palikuwa Kuzimu. Kuzimu ni mahali pabaya sana.

Watu wachache wanafikiri kwamba Kuzimu ni Jehanamu,  lakini wanachanganya kidogo, Kuzimu na Jehanamu siyo sehemu sawa sawa. Jehanamu ni ziwa la moto. Kuzimu ni mahali Mungu alipoumba wakati wa Adamu na inaendelea mpaka hukumu kuu, yaani hukumu ya mwisho. Watu wasiookoka watakwenda Kuzimu na kungojea hukumu.

Biblia ya kiswahili inatumia jina Jehanum yaani Jehanamu mara nane na jina Upotevu mara tisa. Lakini jina Kuzimu Biblia inatumia mara sitini na tisa. Jina Ziwa la moto Biblia inatumia mara chache tu.

  1. KUZIMU

Sasa tunasoma Biblia kuhusu Kuzimu. Tunaona juu ya kuzimu kuna nini na nani anakwenda pale.

[Chaka na hari hukausha maji ya theluji; Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi.] (AYU 24:19)

Tumesoma hivi: [Wamefanya dhambi] wanakwenda Kuzimu. Labda unasema kwamba sisi sote tunafanya dhambi na labda kwa ajili ya dhambi sisi sote tutakwenda Kuzimu pia. Sisi sote tunafanya dhambi, ni kweli, lakini tunajua kwamba Yesu ametoa dhambi zetu na alipata adhabu kwa ajili yetu, kwa hiyo sisi hatuhitaji kwenda Kuzimu. Bwana asifiwe!!

Bali watu wasiookoka wala wasioacha dhambi zao juu ya Yesu, wanakwenda Kuzimu. Yaani waliookoka hawatatumbukizwa pale bali wasiookoka watatumbukizwa Kuzimu.

[Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.  Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.]  (ZAB 49:14,15)

Kabla ya hii inasimuliwa kwamba kuna watu wanaoishi katika dhambi na wanakuwa watumwa wa dhambi. Wao watapelekwa Kuzimu. Lakini katika mstari wa kumi na tano kuna ahadi kwa ajili ya waliookoka: [Mungu atanikomboa nafsi yangu, atanitoa mkononi mwa kuzimu.] Bwana asifiwe!

Sasa tunaona tena kwamba wasiookoka watatumbukizwa Kuzimu lakini waliookoka hapana.

[Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya  mikono yake. Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana. Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa] (ISA 5:11-15)

Tena tumesoma kwamba nani watatumbukizwa Kuzimu. Tumesoma katika mstari wa kumi na moja: [Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!] Na katika mstari wa kumi na mbili Biblia inasema: [.. lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya  mikono yake.]  Tumesoma katika mstari wa kumi na nne kwamba: [Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.]

Mahali gani ni pa Kuzimu? Mstari wa kumi na tano unasema: [Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa.] Kuzimu ni mahali pabaya sana. Mahali pa maumivu na mateso. Natumaini kwamba hata mmoja hatakwenda pale.

[Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, naam, walio wakuu wote wa dunia; huwainua wafalme wote wa mataifa,  watoke katika viti vyao vya enzi. Hao wote watajibu na kukuambia, Je, wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!  Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, na vidudu vinakufunika.] (ISA 14:9-11)

Tulisoma: [Funza wametandazwa chini yako, na vidudu vinakufunika.] Tunaona kuwa huko ni mahali pa kuchukiza. Ikiwa leo hapa kuna mtu ambaye hataki kumfuata Yesu ndiyo sasa unajua utaona nini baada ya kifo chako. Au ikiwa utaacha wokovu wako, sasa ndiyo unajua kwamba milele yako itakuwa baya sana.

  1. PEPONI

Na sasa tunataka kujua kwamba mahali gani ni Peponi. Tumesoma Luka sura ya kumi na sita, mstari wa ishirini na tano, kwamba: [Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. (LK 16:25)  ..na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.]

Wakati wa Lazaro na mtu tajiri walipoishi hapa duniani, maisha ya Lazaro yalikuwa ya huzuni. Alikuwa na njaa. Wakati mwingine alikula chakula pamoja na mbwa. Walikula chakula kilichoanguka chini kutoka juu ya meza ya yule tajiri. Nimeona jinsi wakati wa chakula mifupa inavyotupiwa mbwa. Na vilevile maisha ya Lazaro yalikuwa hivyo. Wakati mwingine Lazaro alipata mifupa kabla ya mbwa, na wakati mwingine mbwa waliipata upesi kuliko Lazaro. Lazaro alikuwa mgonjwa. Alikuwa na vidonda vingi na mbwa wakaja na wakamramba vidonda vyake. Lazaro hakuwa na nyumba yake. Lakini Lazaro alikuwa na jambo moja zaidi kuliko mtu tajiri. Alikuwa ameamini. Amesamehewa na alikwenda kwa Mungu.

Na baadaye watu wote wawili walikufa. Kifo chao kiligeuza hali zao. Lazaro alifikia Peponi. Pale alifarijiwa. Yeye si mgonjwa. Mbwa hawakumramba. Hakula pamoja na mbwa vyakula vile.  Sasa Lazaro alikuwa na hali nzuri sana. Bwana asifiwe!!

Na mtu tajiri, je? Alikuwa vilevile kama Lazaro? Hapana. Wakati wa maisha ya utajiri vitu vyake vyote vilikuwa vizuri. Alikuwa na chakula na nyumba nzuri na alipata alivyotaka. Lakini katika maisha yake hajamtafuta Mungu. Hakusamehewa bali alikwenda kaburini akiwa na dhambi moyoni mwake. Baada ya kufa tajiri sehemu yake ilikuwa mbaya sana.

[Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.] (LK 23:39-43)

Yesu alikuwa msalabani. Yesu alipoadhibiwa yeye aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu. Tulifanya dhambi, si Yesu. Tungalikuwa msalabani wala si Yesu. Lakini Yesu alikwenda mahali petu. Mungu alitupa juu yake dhambi zetu zote. Kwa ajili ya hii dhambi hazikuwa katika sisi bali katika yeye. Dhambi zetu zilipokuwa katika Yesu, aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi, si kwa ajili ya dhambi zake, kwa sababu hana dhambi, lakini aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zako na dhambi zangu. Na sasa tunaweza kuishi katika uhuru, kwa sababu Yesu alitwaa adhabu zetu. Bwana asifiwe!!

Yesu alipokuwa msalabani pia watu wawili walikuwa msalabani karibu naye. Nao ni wahalifu wawili. Wahalifu wawili waliadhibiwa kwa ajili ya makosa yao. Lakini Yesu aliteseka bila ya kuwa na makosa, japo alikuwa katikati ya wahalifu. Kwanza watu wawili hao walimdhihaki Yesu. Mathayo anatusimulia hivi. Lakini walipokuwa msalabani saa chache, mhalifu mwingine alijuta makosa yake alivyoyafanya na akamwambia Yesu:  [Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.] Mhalifu alijua kwamba mtu huyo karibu naye alikuwa Masihi mfalme ambaye amefika kama Agano la Kale lilivyoahidi. Alijua kwamba Biblia inasema kwamba lazima Masihi mfalme atateseka kwa ajili ya dhambi za watu wote. Mhalifu alijua pia, kwamba Masihi mfalme ana ufalme baada ya mauti. Alijuta dhambi zake na aliomba kufika pamoja na Yesu katika ufalme wake. Yesu akamjibu: [Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.]

Baadaye Yesu na wahalifu wawili walikufa. Mhalifu mmoja alikwenda pamoja na Yesu Peponi na mwingine alikwenda Kuzimu.

Tumesoma katika Biblia kwamba Kuzimu ni mahali pa kutisha, pabaya sana. Ni mahali pa kulia. Pale pana maumivu. Watu wasiookoka watakwenda pale pale baada ya mauti yao. Tumesoma pia kwamba Peponi ni mahali pazuri sana. Waliookoka na wanaokufa katika Kristo wanakwenda Peponi. Mhalifu mwingine alikwenda pale na Yesu na labda alimwona Lazaro pia. Mhalifu mwingine alikwenda Kuzimu na labda alimwona mtu tajiri pia.

  1. SHAHIDI KUTOKA KUZIMU NA PEPONI

Kama tungepata shahidi leo kutoka Kuzimu na akaja hapa, tungemwuliza kwamba, je, kuna Kuzimu hivi hivi, kama nilivyowajulisha leo? Angetuambia: Hapana! Hapana! Wewe husemi kweli. Kuzimu ni mahali pabaya sana kuliko unavyojulisha. Angeendelea: Huwezi kusema kwamba ni mahali pabaya. Hakuna maneno yanayotosha hapa duniani kuthibitisha ubaya wa huko.

Au – tungepata shahidi toka Peponi leo na akaja hapa, tungemwuliza kwamba Peponi ni mahali pazuri kama nilivyowajulisha leo, nafikiri kwamba atajibu: Hapana! Hapana! Wewe husemi kweli. Peponi ni mahali pazuri sana kuliko ulivyojulisha. Hakuna maneno yanayotosha hapa duniani kusimulia hali ilivyo huko Peponi.

Leo tumesoma katika Biblia kwamba baada ya mauti waliookoka watakwenda Peponi na wasiookoka watakwenda Kuzimu.

  1. TUPU KUZIMU NA PEPONI

Na sasa tunataka kuuliza: Je, wanakaa pale muda mrefu? Wanaendelea huko milele na milele? Hapana. Hawaendelei milele. Lini wakati wa Kuzimu na Peponi utakwisha? Na baada ya hii itakuwa nini? Paulo alisema: [ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.] (MDO 24:14,15) Kutakuwa na ufufuo wa aina mbili. Nazo ni: Ufufuo wa uzima, na wa hukumu.

Ufufuo wa wafu ni nini? Yaani maiti za watu wote zitafufuka. Mtu atakapokufa maiti yake itazikwa na itakuwa mavumbi tena. Lakini mara moja maiti yake itafufuka. Katika kifo roho ya mtu iliacha mwili wake. Na katika ufufuo roho yake na mwili wake zitakutana tena. Kama mtu amekwenda Peponi baada ya kifo chake, atarudi pamoja na Yesu, wakati wa Yesu atakapofika. Na tena roho na mwili wa mtu vitakutana tena katika ufufuo. Mtu asiyekuwa katika Bwana anapokufa, roho yake itafika Kuzimu. Na mwili wake na roho yake vitakutana tena katika ufufuo wa mwisho. Lakini itatokea wakati mwingine kama ufufuo wa Wakristo. Itatokea kabla ya hukumu ya mwisho.

Hapana mtu atakuwa kaburini milele. Ufufuo wa Wakristo ni mzuri sana kwa waaminio na utatokea wakati wa Yesu atakapofika. Mara nyingi tunahubiri na tunazungumza pia kwamba Yesu atafika. Atachukua watu wake mpaka harusi ya mbinguni. Atakapokuja waaminio wataamshwa kutoka mauti na watapata mwili mpya na watakwenda harusini mbinguni. Watu wasiookoka wataamshwa baadaye. Ufufuo huu si kwa ajili yao. Ufufuo wao utafika baadaye.

[xyz-ihs snippet=”google”]

[Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.] (YN 5:28,29)

Yesu alisema kwamba kuna [ufufuo wa uzima .. na ufufuo wa hukumu.]

Baada ya Yesu atakapokuja yatatokea mambo makubwa mengi. Yataendelea miaka elfu. Sasa siwaelezi mambo ambayo yatatokea katika ufalme wa Kristo. Ufalme wa Kristo utaendelea miaka elfu moja.

  1. HUKUMU YA MWISHO

Baada ya elfu moja kuna hukumu ya mwisho. Mambo ya kuhusu hukumu ya mwisho tusome kitabu cha Ufunuo sura ya ishirini, mstari wa kumi na moja mpaka mstari wa kumi na tano.

[Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu walikuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.] (UFU 20:11-15)

Hii ni hukumu ya mwisho.  Watu wote watafika pale. Wewe utakuwa pale na mimi pia. Watu wote wanaosema kwamba “Mungu hayupo”, watafika. Hapo kuna Waislamu wote na Wakristo pia. Kuna waganga wa kienyeji, wachawi na wanaoabudu roho ya wachafu. Watu wote tangu Adamu mpaka mtu wa mwisho watafika. Tumesoma kwamba: [Bahari ikawatoa wafu walikuwamo ndani yake;] yaani waliokufa maji wasiopata uzishi. Pia tumesoma kwamba: [Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.] Yaani waliokuwa katika Peponi au katika Kuzimu watakuja wote. Wao watahukumiwa.

Tulisoma kwamba kuna vitabu vichache. Kuna vitabu vya Mungu. Katika kitabu hiki kuna vitendo vya watu. Kitabu kingine ni kitabu cha uzima. Katika mstari wa kumi na tano tulisoma: [Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.] Kama jina la mtu lilikuwa katika kitabu cha uzima alifika Mbinguni. Bwana asifiwe!!

Kama jina la mtu hakuwa katika kitabu cha uzima alipelekwa Jehanamu. Majina ya waaminio wote yameandikwa katika kitabu cha uzima. Kitabu cha uzima ni orodha ya waaminio. Jina lako uliyeokoka liko katika kitabu cha uzima. Lakini jina lako usiyeokoka halimo. Wao ambao majina yao hayamo katika kitabu cha uzima walitupwa katika ziwa la moto yaani Jehanamu. Hali ya kuchukiza.

Katika hukumu ya mwisho watu watagawanywa sehemu mbili: watu walioandikwa katika kitabu cha uzima na watu wasio andikwa. Watu wasioandikwa katika kitabu cha uzima watafika mbele ya hakimu. Vitendo vyao vitasomwa katika vitabu vya Mungu. Ambaye amefanya mabaya mengi atapata adhabu kubwa, kubwa kuliko ambaye amefanya mabaya kidogo tu. Lakini wao wote watatupwa katika ziwa la moto yaani Jehanamu kwa sababu majina yao hakuna katika kitabu cha uzima.  Si kwa sababu walifanya dhambi, kwa sababu watu wote wamefanya dhambi, lakini kwa sababu jina halimo katika kitabu cha uzima.

Na pia watu ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima wanasimama mbele ya hakimu. Pia vitendo vyao vitasomwa.

Kumbe, katika vitabu vya Mungu kuna matendo mazuri tu. Hakuna matendo mabaya. Labda watu watauliza kwamba vitendo vyangu vibaya viko wapi? Wataendelea, kwamba nimefanya dhambi, nimekosa mara nyingi. Vitendo vyangu vibaya viko wapi? Hakimu atamjibu kwamba makosa yote na dhambi zote zimetupwa juu ya Yesu,  wakati wa Yesu alipokuwa msalabani na damu yake imesafisha dhambi zako zote kutoka vitabu vya Mungu. Bwana asifiwe!!

Kwa ajili ya hii katika vitabu hivi hakuna makosa wala dhambi. Katika vitabu hivi kuna vitendo vizuri tu. Utapata mshahara kwa ajili ya vitendo vizuri ulivyofanya. Tulisoma, kwamba baada ya hukumu: [iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.] Na watu ambao majina yalikuwa katika kitabu cha uzima watakwenda Mbinguni. Wanakaa Mbinguni milele na milele.

Jina la mtu linaandikwa katika kitabu cha uzima siku ile anapookoka. Tangu siku hiyo yeye ni katika ufalme wa Mungu lakini kwanza anakaa hapa duniani na baadaye huko Mbinguni.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Tulisoma pia katika mstari ya kumi na nne, kwamba [Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto.]  Kwa nini mauti ikatupwa katika ziwa la moto? Kwa sababu mauti haitahitajiwa. Baada ya hukumu hakuna mtu atakayekufa. Milele imeanza. Kwa nini hii Kuzimu ilitupwa katika ziwa la moto? Mungu hahitaji Kuzimu. Sasa kuzimu ni kama jela kwa ajili ya watu wanaokufa bila imani na wanaongoja hukumu ya mwisho. Na Mungu ataiteketeza katika ziwa la moto.

Na Peponi, je?  Mungu anaihitaji? Hapana.

[Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.] (UFU 21:1)

Yohana aliona Mbingu mpya. Mbingu za kwanza zimekwisha. Baada ya hiyo Mungu hahitaji Peponi kwa sababu hakuna mtu atakayefika Peponi baada ya kifo kwa sababu huko Mbinguni hakuna kifo. Kwa ajili ya hii hakuna Peponi. Mungu ameumba Mbingu mpya.

  1. MARUDIO

Na mwisho marudio mafupi: Sasa mtu asiyeokoka atakapokufa atakwenda Kuzimu. Lakini mtu aliyeokoka atakapokufa atakwenda Peponi. Wakati wa hukumu ya mwisho watu wote watafika mbele ya hakimu. Watu waliokaa Kuzimu watakwenda Jehanamu. Lakini watu waliokaa Peponi watakwenda Mbinguni pamoja na Yesu na malaika. Kwa sababu ya umilele, natumaini, kwamba unataka kuishi katika Bwana Yesu na utakuwa pamoja naye milele na milele.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leli/bwiza.com

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.