kwamamaza 7

Askofu awanyanganya waumini kutoka Nyagatare na Gatsibo milioni 16.7

0

Askofu wa Kanisa ya CEPEA Communauté Evangelique de Pentecote de l’Esprit et de l’Amour liloko tarafa ya Simbwa ,wilaya ya Gatsibo anashtakiwa kuwanyanganya waumini wa kanisa yake fedha zinazokadiriwa kuwa milioni 16.7 ya faranga za Rwanda kupitia njia za udanganyifu.

Waumini hawa wapatao 300 wanasema kwamba Askofu huyu aliwadanganya kuwa atatafutia watoto wao maarifa/scholarships ilmradi wamelipa pesa sawa na 65,000 za kujiandikisha kila mmoja katika shirika la Compassion International, shirika la kikristo linalosaidia watoto wasiojiweza kupitia makanisa ya kikristo.

Kwa kuwashawishi waumini hawa kutoa pesa nyingi mno, askofu huyu aliwadanganya kwamba kuna wafadhili kutoka Ulaya wanaokaribia kuwazuru. Raia hawa walichangia pesa nyingi zaidi mojawapo wakauza mali zao. Na mambo yaligeuka walipoona wafadhili hawafiki na kumwita Ngwabije ambaye maelezo yake hakuridhisha waumini na kutoka hapo mzozo ukazuka.

“mpango wa wafadhili kufika hakutekelezeka kwa kuwa Compassion International kwa sasa iko chini ya uongozi wa ADEPR na mnajuwa hatuna uhusiano mzuri. Watoto wenu tumeanza mbinu mpaya ya kuwaandika kupitia kanisa linguine” askofu Ngwabije adai

[xyz-ihs snippet=”google”]

Habari hii inasema pia kuwa kulikuwa wakati Ngwabije alipotumia udanganyifu kama huyu na kuandikisha watoto kupia kanisa la New Life Church ila alizuiwa kwa kosa hili na akaachiliwa huru baadaye.

Ngwabije akijibu haya alisema kuwa yeye ana mpango wakuwapeleka mahakamani waumini wanaosema kuwa amekula fedha zao kwa ajili ya Compassion haana uhusiano wowote na shirika hilo.

Zaidi ya hayo yote hali si nzuri ndani ya Kanisa la CEPEA na hii inahusishwa hususani na uchungaji mbaya wa mali ya kanisa hilo. Na hii inajiri pia wakati viongozi wakanisa la ADEPR wako gereza wakishtakiwa matumizi mabaya na uporaji wa mali ya kanisa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.