kwamamaza 7

Askari jeshi wa Burundi wauawa wengine hutiwa mbaroni

0

Kuwatiya mbaroni askari jeshi wa Burundi imechukuwa hatuwa nyingine, tarehe 24 mwezi huu inajulikana kuwa waliwakamata wanajeshi 18, ila mmoja wao alikutwa ameuawa.

Katika hao wanajeshi kuna wenye ranka ya Luteni na Major, wote walikuwa wakifanya kazi yao katika kambi ya jimbo la Muyinga. Kukamatwa kwao kuna uhusiano na shambulio ambalo lilifanywa  kwenye kambi la Mukoni tarehe 24 Januari 2017.

Tarifa kutoka rfi husema kuwa Adjudant François Nkunzimana aliyekamatwa pamoja na wengine na kupewa polisi, maiti yake iliokotwa akiwa katikati ya maiti mengine ya watu wasiojulikana porini karibu na kambi hio.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Uongozi wa sehemu hio katoa sheria ili waweza kuzikwa katika pori hilo ambao waliuawa wakipigwa risasi.

Gazeti hilo lilijaribu kuongea na kiongozi wa jimbo hata msemaji wa polisi ikashindikana, ila msemaji wa jeshi Col Gaspard Baratuza anahakikisha ya kuwa kuna silaha ambazo ziliibwa katika shambulio la kambi ya Mukoni.

Col Gaspard Baratuza kasema tena ya kuna watu ambao walikamatwa pamoja na wanajeshi, yaliyotokea baadaye hajui kwa kuwa kuna ngazi zingine ambazo huhusika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.