kwamamaza 7

Askari jeshi mkuu ameachana na kundi la FDLR na kurejea Rwanda

0

Mwengine askari mkuu wa wanamgambo wa FDLR ameachana nao na akarudi Rwanda baada ya kushindwa kuishi ubaguzi kati ya kundi hilo. Hayo ni baada ya Gen. Semugeshi kuachana nao na kuingia kundi la CNRD, na hapo ndipo aliamua kukutana MONUSCO na kurejea Rwanda.

Askari huo ana cheo cha Major anajulikana kwa jina la Jean Claude Uwimana alifika Rwanda jana baada ya wiki mbili alipotoroka FDLR katika misitu ya Rutchuru, jimbo la Kivu ya Kaskzini karibu na mji wa Goma na kuwaendea MONUSCO.

Akiwa njiani kwenda MONUSCO, jeshi la Congo FARDC walimukamata na kumutia mbaroni katika kambi lao na alifanya siku kazaa.

Major Jean Claude Uwimana alisema ya kuwa alifikilia kurudi tangu mbele na mwanzo aliwatuma watoto wake wane kutangulia akabaki huko na muke wake sehemu ijulikanao kwa jina la Mweso kama vile husema rwandawire.

Tangu mwaka nenda FDLR ilipoteza wapiganaji wake pakiwemo viongozi, hii huonyesha ya kuwa kundi hilo hupoteza nguvu na kukata tamaa na waliishi misituni karibu miaka 20 wakisema wanapiganisha serikali ya Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya kukamatwa na FARDC alikuwa akiulizwa mahali anapoelekeza na jibu ilikuwa kuwa anaelekeza nchi yake Rwanda, na akiwa pamoja na FARDC ndipo alionana tena na mke wake wakaelekea MONUSCO na wakarahisishiwa kufika Rwanda.

Major Uwimana ni mwenye ukoo wa tarafa ya Mudende, wilaya ya Rubavu, alipokelewa katika kituo cha Mutobo, wilaya ya Musanze, jimbo la Kaskazini na alimukuta Gen Semugeshi aliye wasili Rwanda wiki nenda wakati uongozi wa raia Congo walitamani afikishwe mahakamani nchini akishutumiwa makosa aliyo yafanya akiwa nchini humo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.