kwamamaza 7

Askari Jeshi ameuawa katika mapambano ya M23 na FARDC

0

Jeshi la Congo, FARDC wametangaza ya kuwa walipambana na wapiganaji wa M23 na askari jeshi moja akauawa na wakateka nyara mpiganaji mmoja wa M23.

Mapigano hayo yalifanyika tarehe 20 Februari 2017 katika vijiji vya Tumugenge na Matebe, wilaya ya Rutchuru katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Kituo kinacho husika na upelelezi husema ya kuwa askari wa M23 wapo na lengo la kukaba wilaya ya Masisi ili wapate jinsi ya kupata msaada wa silaha na masasu kama vile husema radio Okapi.

Wakaaji wa wilaya ya Rutchuru wapo na hofu wakikumbuka mauaji walio yafanya wapiganaji wa M23 mwaka wa 2012 na 2013, wakifikiria kuuawa tena.

“Hatutakubali M23 kujikusanya tena kwenye udongo wa Congo, tangu jana askari wa FARDC wanawinda wapiganaji wa M23 sehemu za Jomba, Burayi na Gisigari”. Hayo ni matangazo kutoka kwa kiongozi mkuu wa jeshi anayehusika  na ushambuliaji ujulikanao kwa jina la Sokola II, la kupiganisha wapiganaji katika mji wa Goma.

Hata kama wametangaza hayo, taarifa nyingine husema ya kuwa Gen. Makenga na jeshi lake wapo katika Kivu ya Kaskazini, wilaya ya Rutchuru.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.